Header Ads Widget

MBEGU BORA ZA MUHOGO- "ONGEZA TIJA MUHOGO UNALIPA"

 


Wakulima wamehasishwa kutumia mbegu bora za muhogo zilizo fanyiwa utafiti na taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania(TARI) kupitia kituo cha Ukiriguru.

Hii ni kufatia SIKU YA MKULIMA iliyoendeshwa mkoani Kagera, wilayani Bihalamlo, kata ya Runazi kijiji cha Runazi mapema leo tarehe 15.11.2022.



Jumla ya aina tisa(9)za mbegu bora za mihogo zilizofanyiwa utafiti na zinazokinzana na ugonjwa wa batobato na michilizi kahawia zimeshuhudiwa na wakulima. Mbegu hizo ni pamoja na:-TARICASS1, TARICASS 2, TARICASS 2, TARICASS 3, TARICASS 4, TARICASS 5, KIROBA na MKUMBA.



Aidha, wakulima wamepata nafasi ya kujifunza kanuni za kilimo bora cha zao la muhogo, namna ya kukabiriana na magonjwa ya za zao la muhogo pamoja na faidi kwa ujumla za zao la muhogo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI