Header Ads Widget

DKT MWINYI AMEFANIKIWA KUWAUNGANISHA WAZANZIBAR KUPITIA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA- MZEE BARAKA SHAMTE

 




NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR


MWANASIASA Mkongwe Visiwani Zanzibar Mzee Baraka Shamte amesema kuwa, Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoongozwa na Rais Dkt Husssein Ali Mwinyi imefanikiwa kuwaunganisha Wananchi visiwani humo pamoja na Zanzibar kuwa katika hali ya Utulivu.


Ameyasema hayo jana wakati atitoa mada katika Mkutano kwa njia ya Mtandao ambao ulikuwa unajadili tathimini ya Uongozi wa Dkt Hussein Ali Mwinyi katika kuimarisha Demokrasia na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambapo amesema kwamba tangu kuingia madarakani kwa Rais Dkt Hussein Mwinyi mashirikiano na utulivu wa Nchi umezidi kuimarika Visiwani.


Amesema matukio ya watu kupigwa pamoja na kuripotiwa kwa vcisa mbalimbali vimepugua Visiwani ambapo watu wanaishi kwa Amani na Utulivu huku wakishirikiana katika Nyanja zote za Kijamii.


“Watu wa Zanzibar wanashirikiana katika shughuli za Kijamii kama vile kuzikana hapo awali watu walikuwa wakiishi bila ya kuzikana na kushirikiana katika shughuli za kijamii, Tunatakiwa kumpongeza Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa dhamira yake ya kuwaunganisha Watu pamoja,” amesema.


Ameeleza kuwa, Dhamira ya Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni njema ambapo ndani ya Serikali yake anawashirikisha vyama vya vya upinzani mbali na vyama viwili ACT Wazalendo na CCM.


“Serikali ya Umoja wa Kitaifa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo Rais amekuwa akiwashirikisha vyama vingine mbali na CCM na ACT Wazalendo ambao wao ndio wanaunga Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” ameeleza.


Hata hivyo ameeleza kwamba Makamu wa kwanza wa Rais bado hajawa na Uwezo wa Kumshauri Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi badala yake anapita Nje na kuanza kurusha Maneno.


“Mhe Makamu wa Kwanza wa Rais bado hana uwezo wa Kumshauri Rais maana yeye anashiriki katika baraza la Mapinduzi lakini pia yeye ana uwezo wa kuzngumza nae faragha kwa kumshauri mambo mbalimbali kwa Maslah ya Taifa lakin bado hajawa na ujasiri wa kuweza kumshauri Rais Dkt Hussein Mwinyi,” ameongeza.


Mkutano huo umehudhuriwa na Mamia ya Wananchi kutoka Zanzibar na Tanzania bara ambao ulikuwa unajadilia tathimini ya Uongozi wa Dkt Hussein Ali Mwinyi katika kuimarisha Demokrasia na Serikali ya Umoja wa Kitaifa

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI