Header Ads Widget

MADIWANI MAKETE WAKUMBWA NA HOFU JUU YA UJENZI WA BARABARA

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mkoani Njombe wameelezea wasiwasi wao kuhusu matengenezo ya barabara kuchelewa kuanza kutokana na msimu wa mvua kuwadia.


Katika Kikao cha Baraza la madiwani wilayani humo baadhi ya  madiwani hao akiwemo Osmund  Idawa na Raymond Mgaya pia wameelezea masikitiko yao ya barabara kutengenezwa kwa vipande vifupi vifupi na kusema hali hiyo ni kama haileti tija.



Mhandisi John Kawogo kutoka   TARURA wilaya ya Makete ametolea ufafanuzi huo kuwa fedha zinazotolewa ni kwa ajili ya matengenezo na fedha hizo zinakuja kidogo tofauti na walivyopanga kwenye bajeti.


Kuhusu Barabara ya Lupila Kipengere amesema  baada ya mkandarasi kumaliza kutengeneza barabara ya Ibaga alikwenda Luwumbu na kwa sasa amebakiwa na mradi huo wa barabara ya Lupila Kipengere hivyo atakwenda kuitengeneza barabara hiyo.


Hawa Ahmad ni Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye amemtaka Meneja wa TARURA Kuyafanyia kazi mapendekezo na ushauri uliotolewa na baraza hilo huku akimtaka kutoa vipaumbele kwenye  barabara ambazo hazipitiki kwa kuwa sio mgeni na barabara za wilaya ya Makete.



Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Makete William Makufwe ameishauri TARURA kutoa zabuni kwa wakandarasi wengi badala ya mkandarasi mmoja kupewa barabara nyingi hali inayochangia matengenezo ya barabara hizo kuchelewa kuanza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI