Header Ads Widget

KJP YAZINDUA AWAMU YA PILI UTEKELEZAJI MIRADI YA WANANCHI KIGOMA.

 

Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye (wa pili kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Zlatan Milisic (wa pili kushoto) wakifungua Pazia ikiwa ishara ya uzinduzi rasmi wa awamu ya pili ya mpango wa Pamoja Kigoma (KJP) unaitekelezwa kwa pamoja na serikali na mashirika 16 ya Umoja wa Mataifa

(Picha na Fadhili Abdallah)

Mwakilishi mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Zlatan Milisic akizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango wa pamoja Kigoma unaotekelezwa na Mashirika 16 ya Umoja wa Mataifa
(Picha na Fadhili Abdallah)
Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye (kulia) akitoa salamu za serikali katika hafla ya uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango wa pamoja (KJP) unaitekelezwa na mashirika 16 ya Umoja wa Mataifa
(Picha na Fadhili Abdallah)
Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa mataifa na mabalozi wa nchi wafadhili wakifuatilia uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango wa pamoja Kigoma unaotekelezwa na mashirika 16 ya Umoja wa Mataifa.
(Picha na Fadhili Abdallah)

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

UMOJA wa Mataifa umezindua awamu ya pili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi kupitia mpango wa pamoja wa Kigoma (KJP) unaotekelezwa na Mashirika 16 ya Umoja wa Mataifa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango huo uzinduzi uliofanyika mjini Kigoma Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini,Zlatan Milisic alisema kuwa Umoja wa Mataifa umeongeza utekelezaji wa mpango huo kwa miaka mingine mitano.

Milisic alisema kuwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi unaotekelezwa na mashirika 16 ya  Umoja wa Mataifa unafuatia mafanikio makubwa ambayo mpango huo imeupata katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mpango huo.

Mwakilishi huyo alisema kuwa katika awamu hii ya pili wanatarajia kuwafikia watu 400,000 kutoka wilaya zote za mkoa Kigoma.

Mwakilishi huyo alisema kuwa katika awamu hii pili mpango huo utatumia kiasi cha dola milioni 2.5 kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mkuu wa mkoa Kigoma, Thobias Andengenye alisema kuwa serikali imefarijika kwa kiasi kikubwa kwa Umoja wa Mataifa kuongeza awamu nyingine ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi kupitia mpango wa pamoja Kigoma (KJP).

Andengenye ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa kamati ya Usimamizi ya KJP alisema kuwa awamu ya kwanza ya mpango huu kumekuwa na mafanikio makubwa hasa katika kusaidia serikali kutekeleza mipango ya maendeleo ya wananchi.

Andengenye alisema kuwa awamu hii ya pili miradi imejikita katika vipaumbele vya changamoto na mahitaji yaliyopo kwa wananchi hivyo miradi itakayotekelezwa inagusa moja kwa moja maisha ya wananchi wa kawaida.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI