Header Ads Widget

KATIBU MWENEZI CCM NJOMBE ERASTO NGOLE AFUNGUKA JINA LAKE KUKATWA UNEC


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Baada ya halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi ccm taifa kuteua majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali zikiwemo za jumuiya taifa na mikoa,Katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Njombe Erasto Ngole ambaye jina lake pia limekatwa kwenye nafasi ya ujumbe wa halmashauri kuu taifa[NEC] amekiri kupokea taarifa hizo na kwamba atasalia kuwa mwanachama imara.


Akizungumza na vyombo vya habari Ngole amesema hakuna sababu ya kukichukia chama kwa kukatwa jina lake hivyo anaheshimu maamuzi yaliyofanyika kwa maslahi mapana ya chama na serikali.


Duru zinaeleza kuwa nafasi ya uenezi ngazi ya mkoa imefutwa na badala yake zitatolewa ajira ambapo Ngole ambaye atasalia kuwa mwenezi wa chama mpaka mwezi machi mwakani anasema ataendelea kupokea maelekezo yatakayokuwa yakitolewa huku akisema hawezi kuajiriwa kwa umri wake alionao hivi sasa.



Katibu wa umoja wa vijana UVCCM Mkoa wa Njombe Hamis Ally Kachinga yeye amesema baada ya majina matatu kurejea kwenye nafasi mbalimbali ndani ya jumuiya wanatarajia kufanya uchaguzi hapo novemba 16 mwaka huu na kuonya udanganyifu,rushwa na fitina katika mchakato huo.



Kituo hiki kimelazimika kumtafuta mmoja wa wagombea uenyekiti wa UVCCM Mkoa ambaye jina lake limerejeshwa bwana Samuel Mgaya ambaye amesema amepokea maamuzi ya chama taifa kwa mikono miwili na kuahidi kwenda kwenye uchaguzi akiwa muumini wa siasa safi.



Baadhi ya vijana akiwemo Hamis Hassan Kassapa wanasema kwenda kuchagua viongozi kwa njia ya rushwa kunaweza kuleta madhara makubwa ndani ya taifa.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS