Header Ads Widget

PAC: YATEMBELEA MRADI WA JNHPP


Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali (PAC) imefanya ukaguzi ili kuona maendeleo ya ujenzi wa mradi Mkubwa wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere Hydropower Project ambao unatekelezwa na Serikali kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa nishati ya umeme nchini 


Akizungumza katika ziara iliyofanyika Novemba 13, 2022, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka alisema kuwa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali imefanya ziara ya kutembelea mradi huo ili kutazama thamani ya Fedha iliyotumika katika utekeleza wa mradi wa JNHPP.


“Niseme sisi kama Kamati ya Kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali tunaipongeza Wizara kwa kufanikisha ziara ya kamati na tumeiagiza Wizara kwenda kuzifanyia kazi hoja zilizotolewa na wajumbe baada ya kukagua na kuona maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa, ambao umefikia asilimia 74 za ujenzi.


Hata hivyo, baadhi ya hoja zilizotolewa na wajumbe wa kamati ili zikafanyiwe kazi na Wizara kabla ya kufika mwezi January, 2023 ni kutaka kufahamu gharama halisi ya utekelezaji wa Mradi mzima yaani kuanzia kuzalisha umeme,kupoza na  kusafirisha pamoja na kuwepo kwa tozo maalumu kwa ajili ya kuhifadhi mazingira yanayozunguka mradi wa JNHPP.


Aidha, Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, alisema kuwa hoja zote zilizowasilishwa na wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali, mara baada ya kufanya ukaguzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa Julias Nyerere (JNHPP) zitafanyiwa kazi na majibu ya hoja hizo yatawasilishwa Kwa maandishi ndani ya siku 14 kwa kamati husika kama ilivyoagizwa. 


Pia, Byabato alisema kuwa shirika la umeme nchini (TANESCO) lipo kwenye Mpango wa kuanza kuhifadhi mazingira kwa kusimamia na kupanda miti katika maeneo yote yatakayoleta Maji  katika mradi wa JNHPP ili kuendelea kuhifadhi mazingira.












Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS