Header Ads Widget

WANNE WAKAMATWA NA KILO 53 ZA DHAHABU INDIA WAKITOKEA TANZANIA


Raia wanne wenye asili ya Asia waliokuwa wakisafiri kutoka Tanzania kwenda nchini India, wanashikiliwa na Mamlaka za Uwanja wa Ndege wa mjini Mumbai, baada ya kukamatwa na kilo 53 za dhahabu walizokuwa wamezificha. 


Watuhumiwa hao walikutwa na dhahabu hizo zinazotajwa kuwa na thamani ya Shilingi bilioni nane(8) walizokuwa wameficha kwenye mikanda maalum iliyokuwa na mifuko ya kuhifadhi kilo moja moja za madini hayo. 


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na maafisa wa forodha katika uwanja huo, dhahabu zimekamatwa pamoja na mzigo mwingine wa kilo nane kutoka kwa abiria wengine watatu waliokuwa wakisafiri kutoka Dubai. 


Tukio hilo linaelezwa kuwa kubwa zaidi kutokea kwa siku moja katika uwanja huo wa kimataifa na jumla ya dhahabu iliyokamatwa ni kilo 61 zenye thamani ya Shilingi bilioni tisa(9).

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS