Na MWANDISHI WETU, ZANZIBAR
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini Ameir Hassan Ameir amewataka Vyama vya Siasa pamoja na Wanasiasa Nchini kuhakikisha Wanalinda na kuenzi Amani na Utulivu uliopo sasa Visiwani Zanzibar.
Amesema Vyama vya Siasa na Wanasiasa wanawajibu huo ambapo ni vyema kwa kuhakikisha kila siku wanahubiri namna ya kulinda na kuenzi Amani, Umoja na Mshikamano wa Wazanzibar.
Hayo ameyaeleza leo katika Mkutano kwa njia ya Mtandano wa ZOOM ambao ulikuwa na unajadili tathimni ya Uongozi wa Dkt Hussein Ali Mwinyi katika kuimarisha Demokrasia na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambapo amesema kwamba vyama vya siasa vina makundi makubwa ya watu wanaowasikiliza hivyo ni vyema kwao kushajihisha kulinda amani ya Nchi.
“Sisi Wanasiasa tuna dhima ya kuhakikisha Amani ya Nchi inalindwa kwa gharama yoyote ile, Wito wangu kwa Wanasiasa tutimize wajibu wetu kwa kuhakikisha huu Umoja tuliokuwa nao unaendelea, hii Amani ya Zanzibar inalindwa kwa gharama yoyote ile,” Amesema.
Aidha Katibu Ameir ametoa wito kwa Wanachi Visiwani Zanzibar kuwa wasikubali kuyumbishwa kwa kusikiliza kauli za Wanasiasa ambao hawana dhamira njema ya Zanzibar.
Amesema Wananchi visiwani humo wanapaswa kuwalaani vikali wanasiasa ambao dhamira yao ni kuwagawa Wananchi kwa kauli zao na Misingi yoyote ile.
“Sio dhambi kuvikataa vyama visivyokuwa na dhamira njema,sio dhambi kuwaalaani vikali na kuwakata Wanasiasa wenye nia ovu na Zanzibar,”ameeleza.






0 Comments