Header Ads Widget

DIWANI ATAKA FEDHA M 800 ZITUMIKE KUKAMILISHA HOSPITALI



 DIWANI wa Kata ya Picha Karim Mtambo ameitaka Halmashauri ya Mji wa Kibaha kuzitumia milioni 800 ambazo zilitengwa kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Lulanzi.


Akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo alisema kuwa inashangaza kuona kuwa hadi sasa ni miezi sita fedha hizo hazitumiki kukamilisha ujenzi.


Mtambo alisema kuwa hakuna sababu ya kushindwa kuzitumia fedha hizo ambazo zipo kwa ajili ya kazi hiyo tatizo liko wapi hii fedha itakwenda na watu.


"Bajeti iliyopita tulisomewa nashangaa hadi leo tena tunasomewa kuwa fedha hizo bado zipo na hazijafanyiwa kazi tunataka zitumike ili mradi huo ukamilike na huduma ziendelee kuboreshwa,"alisema Mtambo.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde alisema kuwa mradi huo una awamu mbili ambapo hatua ya kwanza zilitumika milioni 500 na awamu ya pili zimetumika milioni 400 kati ya milioni 800 ambapo changamoto ni kamati ya ujenzi kuhofia kutumia fedha kwa ajili ya ununuzi wa maji ambapo bajeti yake haikuwepo.


Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Musa Ndomba alisema kuwa inashangaza kuona bajeti ya maji haiwekwi kisa haikuwepo kwenye bajeti maji ni kama vifaa vingine hivyo bajeti yake lazima iwepo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI