Header Ads Widget

CHUO WAOMBA SERIKALI KUTOA UFADHILI WA VYUO VYA KATI.

Mkuu wa hospitali kuu ya jeshi mkoani Tabora Dkt Luteni Kanali Dkt  Mikidadi Magogo akizungumza na jumuiya ya wanachuo wa chuo Cha Afya Cha Mtakatifu Maximilliancolbe.

Mkurugenzi wa Chuo Cha Afya Cha Mtakatifu Maximilliancolbe Elizabeth Nkonyoka akitoa wito kwa wanachuo waliomaliza miaka 3 ya kozi ya utabibu na ufamasia .

Wanachuo wa Chuo Cha Afya Cha Mtakatifu Maximilliancolbe wanaohitimu kozi ya utabibu na ufamasia wakifurahia jambo mbele ya mgeni Rasmi..

Wanachuo wa Chuo Cha Afya Cha Mtakatifu Maximilliancolbe katika Picha ya pamoja katika viwanja vya chuo hicho.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Lucas Raphael,Tabora

 Chuo Cha Afya Cha Mtakatifu Maximilliancolbe cha mkoani Tabora  wameiomba Serikali kuwapatia  ufadhili wa masomo kwa vyuo vya kati nchini ili wanavyuo wengi waweze kusoma kama ilivyo vyuo vikuu nchini.

 

Mkurungezi wa chuo hicho Elizabeth Nkonyoka alitoa kauli hiyo jana katika  Mahafali ya Pili ya chuo cha St. Maximilliancolbe yaliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho Mkoani Tabora .

 

Alisema kwamba kutokana na mahitaji ya wanafunzi kusoma katika fani mbalimbali wanashindwa kutokana na kukosa ada ,hivyo kuiomba serikali kuwapatia ufadhili kwa vyuo vya kati nchini.

 

Elizabeth alisema kuwa  wengi wa wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivyo hawana uwezo kuendelea na masomo kutokana na ada ya masomo kuwa kubwa na hivyo kukatisha ndoto zao za kupata elimu bora.

 

“wanaiomba Serikali ya awamu ya sita iweze kuwasaidia watoto wanaotoka katika mazingira duni na kuwasaidia kuona jinsi ya kuwasaidia kupata mikopo kwenye vyuo vya elimu ya Kati”alisema Elizabeth Nkonyoka


Mkurugenzi huyo wa chuo hicho alisema kwamba kutokana na ufadhili huu ,wahitaji wa misaada  ni wengi sana na gharama za uendeshaji kuwa ni kubwa sana na  changamoto hiyo inapelekea watoto wengi kuahirisha masomo au kuacha kabisa masomo na kusababisha kukatisha ndoto zao.

 

Elizabeth alisema kwamba Chuo hicho kimefanikiwa kuwadhamini wanafunzi 25 wenye uwezo mzuri darasani , ambao wanatoka katika familia duni na walioshindwa kumudu kulipa gharama za masomo chuoni hapa kwa kuwalipia gharama zote.

 

Awali mgeni rasmi kutoka hospitali kuu ya jeshi mkoani Tabora Dkt  Luteni Kanali Dkt  Mikidadi Magogo aliupongeza uongozi wa chuo hicho  kwa kutoa elimu bure kwa wanafunzi  25 ambao wataweza kupatikana Madaktari wazuri wenye elimu ya kutosha.


Aliwataka wanafunzi wanaomaliza chuo huko  waendako wakafanye kazi kwa weledi na kuwaonea huruma wagonjwa wanaofikishwa katika vituo vyao vya kazi.


Aidha aliwaasa wahitimu hao kuwa na tabia nzuri huko waendako na sio kuharibu cheti chao kwa kupewa sifa mbaya.


Alisema ajira ni wao wenyewe watakapoamua kuchakalika na sio lazima kusubiria ajira za Serikali Kuna taasisi nyingi zinahitaji watabibu na wafamasi kama wao .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI