Na Editha Karlo,Matukio Daima Kigoma
Abdukadiri Daudi Mushi amechaguliwa kua mjumbe wa Halmashauri kuu chama cha mapinduzi Taifa(MNEC)Mkoa wa kigoma baada ya kuwashinda wagombea wenzake wawili.
Mushi ambaye alikuwa anatetea kiti chake,akitangaza matokeo ya uchaguzi msimamizi wa uchaguzi huo Balozi Batrida Burian ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Tabora alisema kuwa mshindi alipata kura 645.
Alisema jumla ya kura 836 zilipigwa zilizoharibika zilikuwa kura 2 huku kura halali zikiwa 835,ambapo mshindi wa pili Shauri Kayandabila alipata kura 105 na mshindi wa tatu Injia Mussa Issa Sasilo alipata kura 57
Mushi aliwashukuru wajumbe kwa kuwa na imani naye nakumpa kura za kishindo atahakikisha anasimamia vyema miradi ya chama ikamilike kwa wakati ili ilete maendeleo kwa wananchi.
‘’Ndugu zangu mnanifahamu mimi huwa ni mtu wa vitendo siyo maneno,Uchaguzi umekwisha sasa tunakwenda kujenga chama chetu kiwa wamoja hakuna tena yale mambo wakati wa kutafuta kura,sasa ni wakati kufanya kazi na si maneno tena’’Alisema Kadri
0 Comments