Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
Hayo ya yamebainishwa leo Octoba 7,2022 na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini , Mhandisi Yahya Samamba Wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa alipokuwa akieleza vipaumbele vya Taasisi kwa mwaka was fedha 2022/2023.
Mhandisi Samamba Alisema Mwaka 2021, mchango wa sekta ya madini kwenye Pato la Taifa ulikuwa asilimia 7.3 kutoka asilimia 4.8 mwaka 2018. Lengo likiwa kufikia asilimia 10 ifikapo 2025.
Alisema ukuaji wa sekta ya madini mwaka 2021 ulikua kwa asilimia 9.6 ukilinganisha na ukuaji wa asilimia1.5 mwaka 2018.
Aidha, jumla ya mitambo mitatu ya kusafishia dhahabu imejengwa na mashine 23 za kuongeza thamani madini zimekamilika.
"Katika kipindi cha mwaka 2018-2021, Tume imesimamia vyema suala la usalama, afya, mazingira na matumizi ya baruti migodini kwa kushirikiana na taasisi zingine. Jumla ya migodi 141 mikubwa, kati na midogo ilikaguliwa," Alisema
Hata hivyo Mchango wa wachimbaji wadogo kwenye mapato yanayokusanywa na Tume umeimarika hadi kufikia asilimia 30 mwaka 2021 ikilinganishwa na chini ya asilimia 24mwaka 2018.
Alisema Tume imejipanga vizuri kusimamia ipasavyo miradi yote ya madini itakayozalisha nishati safi kwa ajili ya utengenezaji wa betri za magari, nishati ya kuendeshea mitambo mikubwa na madini yatakayotumika katika teknolojia kubwa.
Kuanzia mwaka 2019, Serikali imefanikiwa kuanzisha jumla ya masoko ya madini 42 na vituo vidogo vya ununuzi 83. Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 masoko na vituo hivyo vimechangia Shilingi bilioni 164.09 ukilinganisha bilioni 145.23 kwa mwaka 2020/2021.
VIPAUMBELE VYA TAASISI KATIKA BAJETI YA MWAKA 2022/2023
Alisema Kukusanya Shilingi bilioni 822, kufuta leseni zote ambazo haziendelezwi kusimamia ipasavyo miradi ya madini, kuimarisha zaidi hali ya usalama, afya na mazingira ya migodi.
Alisema Kipaumbele kingine ni kuendelea kufungamanisha sekta ya madini na sekta zingine, kusimamia ipasavyo ushiriki wa wazawa, kuendelea kuvutia wawekezaji, kuzuia kupambana na utoroshaji na biashara haramu ya madini na kuendelea kutoa elimu kwa umma na wawekezaji.
Kwa Upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa Alisema Nchi ya Tanzania ni moja ya nchi ambazo zimejaaliwa na Mungu kuwa na utajiri mkubwa wa madini, tunachokifanya ni kutafiti kufahamu yalipo ili yaweze kunufaisha nchi, katika kutekeleza hili tunashirikiana na sekta binafsi.
Alisema Mtazamo wa Serikali kwa sasa ni kupanua wigo wa kunufaika na madini kwa sababu tumefanya utafiti wa kubaini madini yetu kwa asilimia16 tu, hivyo tunataka tujadiliane na wadau ili kuchimba maeneo mengi zaidi.
"Tunataka tufanye utafiti wa kina kujua madini mengi zaidi angalau kufikia asilimia 40 ili Serikali ijenge mazingira mazuri na kuzihamasisha sekta binafsi kuchimba madini hayo," Alisema Msigwa.
0 Comments