Header Ads Widget

WAZIRI MKUU KASSIMU MAJALIWA KUKAGUA MIRADI NANE MKOANI MWANZA

 


NA CHAUSIKU SAID,MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.

Waziri Mkuu Kassimu Majliwa anatarajiwa kufanya ziara Mkoani Mwanza na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ufunguzi wa jengo la huduma ya macho katika hospitali ya Kanda ya rufaa Bugando.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adamu Malima alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  juu ya ujio wa Waziri Mkuu na kueleza kuwa atafanya ziara yake siku nne (4) yenye lengo la kukagua miradi mbalimbali katika wilaya za Mkoa huo.

 Malima ameeleza kuwa Mhe Waziri Mkuu atatembelea na atakagua Daraja la Magufuli lililopo Kigongo Busisi na kujionea namna ujenzi huo unavyoendelea pamoja na ukaguzi wa Stendi ya Mabasi Nyegezi na  meli ya MV Mwanza hapa kazi tu baada ya ujenzi wake kuwa unasuasua na kutoa maagizo makali ya meli hiyo kukamilika kwa wakati.

"Sisi wote tunafahamu Mara ya mwisho Waziri Mkuu alipokuja Mwanza alikwenda kutembelea ujenzi wa meli hiyo na kukuta ujenzi wake unasuasua na kutoa maagizo makali sana juu ya ujenzi huo kukamilika" Alisema Adamu.

Amefafanua kuwa Kassimu atapata wasaha wa kusalimiana na wananchi ataelekea  wilayani Kwimba  kukagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na kujionea namna ya utekelezaji wake unavyokwenda.

Oktoba 17 Majaliwa  atakagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo Cha Afya Irugwa  na baadaye atakagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Irugwa ambapo baada ya ukaguzi huo, ataelekea kisiwa cha Gana kukagua ujenzi wa zahanati ya Gana hatua ya msingi.

Aidha Malima amewataka wananchi wa mkoani Mwanza kujitokeza kwa wingi barabarani ili kuweza  kumpokea Waziri Mkuu kama ilivyo jadi ya wana Mwanza  kuwa na ukarimu Kwa wageni.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI