Header Ads Widget

WAZIRI MABULA ASISITIZA WATHAMINISHAJI UZALENDO WA UTHAMINISHAJI WA MALI ZA WANANCHI

 

Teddy Kilanga, Arusha

Waziri wa Ardhi,nyumba na maendeleo ya Makazi,Angeline Mabula wamewataka wataalamu wa uthaminishaji mali wasiokuwa waaminifu nchini kuacha tabia ya kuwalaghai wananchi  na Taasisi mbalimbali juu ya uthamini wa mali katika hitaji ya huduma  za mikopo na ardhi.


Akizungumza jijini Arusha Oktoba 20,2022,wakati akifungua mkutano wa tatu  wa bodi ya usajili wa Uthamini, Mabula amesema serikali imegundua  tabia ya baadhi ya wathaminishaji kuwalaghai wananchi kwa  kupandisha thamani ili kusaidia upatikanaji wa mkopo haraka  na inapofikia muhusika kashindwa kulipa fedha hizo haipatikani kwa kiasi kilichothaminiwa.


Mabula alisema kitendo hicho ni utovu wa nidhamu na ukiukwaji wa taaluma ya kazi kwani kinachafua taswira kwa wananchi hali inayosababisha wizara kuwa na migogoro mingi.


"Hapa kuna changamoto kubwa hasa kwa  wathamini wa taasisi za benki hivyo naomba sana watu wa taasisi hizi waelewe na kuweza kuisaidia serikali kwani kumekuwa na ukiukwaji wa haki hali inayozalisha migogoro baina ya wananchi na benki,"amesema Mabula.


Mabula amesema hapa nchini kuna vitendo vya aina nyingi ambavyo vinachafua taaluma ya uthaminishaji nakuisababishia wizara kuwa na migogoro mingi hususani ya fidia na malalamiko ya kukwama kwa miamala ya ardhi mfano uhamisho wa benki.


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Dkt.Allan Kijazi alisisitiza ushirikiano baina ya sekta binafsi na serikali ili kuondoa migogoro ya upangaji wa gharama ya uthaminishaji mali na kuleta tija katika utendaji wa kazi zao.


"Na hii itatusaidia kujenga umoja,ushirikiano na kuweza kufanya kazi zetu kitaalamu zaidi ambapo tutaweza kuwahudumia watanzania kwa tija kuliko ambapo tunafanya sasa hivi,"amesema Dkt.Kijaji.


Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongela amesema sekta hiyo ya uthamini inasaidia katila kuchangia maendeleo kutokana na kila mali za mwananchi zinahitaji kuthaminiwa ili viweze kujulikana ikiwemo uwekezaji na katika mkoa huo wanayokazi ya kuchagiza uwekezaji.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya usajili wa wathamini,Cletus Ndjovu amesema kutokana na utovu wa nidhamu Mthamini mmoja amefungiwa na kampuni za usajili tano  zimepigwa faini kwa viwango mbalimbali ikiwa watatu wamepewa onyo.


"Bodi imefanikiwa kupokea na kufanyia kazi  yanahusu maadili ya kazi za uthamini kutoka kwa Mthamini mkuu na wathamini wengine pamoja na umma  na katika kutimiza majukumu hayo wamechukua hatua mbalimbali za kukomesha wale wanaoenda kinyume na maadili ya kazi,"alisema Mwenyekiti huyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI