Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima amevitaka vyama vya Ushirika kuwa na nguvu zaidi ili viweze kuanzisha Benki ya Taifa ya Ushirika na kuiomba Serikali kuweza kusaidia vyama hivyo katika uanzishwaji wa benki hiyo ambapo kiasi cha shilingi bilioni 15 zikitajika katika uanzishwaji wake
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Akiba na Mikopo Tanzania Eng.Dkt Cuthbert Msuya ( SCCULT 1992 LTD ) amesema, SACCOS zimechangia katika kuboresha maisha ya jamii kwa kuwawezesha wanachama,kupata mitaji,kugharamia elimu kwa watoto wao,kumudu gharama za afya,kumiliki vyombo vya usafiri navifaa mbalimbali pamoja na makazi boraMrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini Dkt.Benson Ndiege, amesema bado kuna changamoto katika utoaji wa taarifa za ukaguzi kutokana na kutokuwepo usimamizi makini wa mali za ushirika huku akitupia lawama kwa mameneja wa vyama vya akiba na mikopo huku akiahidi kuchukuliwa sheria kwa kushindwa kusimamia mali za wanaushirika



.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)





0 Comments