Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika
la Plan International Dkt. Mona Girgis ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma leo
Oktoba 26, 2022. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew Komba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akikabidhi Mkakakati wa Kitaifa wa Mbadiliko ya Tabianchi wa mwaka 2021-2026 kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Plan International Dkt. Mona Girgis mara baada ya kufanya nae mazungumzo ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma leo Oktoba 26, 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Plan International Dkt. Mona Girgis, Mkurugenzi (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew Komba (kushoto), Bi. Zuhura Mbura na Bi. Secilia Bosco na kutoka Plan International mara baada ya kikao ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma leo Oktoba 26, 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiagana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
Plan International Dkt. Mona Girgis mara baada ya kufanya mazungumzo ofisini
kwake Mtumba jijini Dodoma leo Oktoba 26, 2022.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Plan International Dkt. Mona Girgis ofisini
kwake Mtumba jijini Dodoma leo Oktoba 26, 2022.
Katika mazungumzo yao Dkt. Mona na aliyeambatana na Ujumbe wake aliwasilishaprogramu ya utekelezaji wa majukumu ya shirika hilo hapa nchini yakiwemo ulinzi wa mtoto, maji na usafi wa mazingira.
Pia alimuelezea Waziri
namna Plan International inavyoshiriki katika jitihada za mapambano dhidi ya
athari za mabadiliko ya tabianchi zinazokumba Tanzania na dunia kwa ujumla.
Alisema shirika hilo
linatarajia kushiriki katika Mkutano wa 27 wa Nchi
Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi
unaotarajiwa kufanyika nchini Misri Novemba 2022.
Waziri Jafo alipongeza jitihada za shirika hilo za kuunga
mkono Serikali katika uhifadhi wa mazingira ikiwemo kukabiliana na athari za
mabadiliko ya tabianchi.
Alisema Serikali itakuwa bega kwa bega na washirika wa
maendeleo wakiwemo Plan International ili kuimiza malengo ya kuhakikisha hali
ya uhifadhi wa mazingira inaimarika.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi Dkt. Andrew Komba, Mtaalamu wa Mawasiliano na Uchechemuzi Bi. Cesilia Bosco na Mtalaamu wa masuala ya Uchechemuzi Zuhura Mbura kutoka Shirika la Plan International.





0 Comments