Na Zulfa Alfan matukio daima App .simiyu.
Waziri wa kilimo Hussein Bashe amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kutowagawia wakulima RUZUKU ambao hawatojisajili Katika daftari la kilimo ili
Waziri wa kilimo Hussein Bashe amewataka wakulima kujisajili na kutoka taarifa sahihi Katika daftari la kilimo Ili waweza kunufaika na zuruku zinazotolewa na serikali.
Waziri Bashe ameyasema hayo Katika kilele cha wiki ya chakula duniani ambapo kitaifa yamefanyika mkoani simiyu.
Aidha waziri Bashe amewaomba wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kutowagawia wakulima ambao hawatojisajili Katika daftari la kilimo kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kujua idadi ya wakulima waonatakiwa kupatawa RUZUKU za kilimo Kama vile dawa,mbegu na mbolea.
"Niwaombe wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa msimgawie mkulima yeyote ambae hajasajiliwa Katika daftari la kilimo Ili tumjue siku ya mwisho isijeikawa dawa tunazogawa zinaishia kwenye maduka" Amesema waziri Bashe.
"Ili RUZUKU zenu zisitapeliwe mjisajili na mtoe taarifa sahihi na namba yako ya simu Ili sikumoja nikikupigia simu nakuuliza fulani umepata mbolea kwa wakala kwasababu umesajiliwa na ukisajiliwa utapata namba ya siri usimpe mtu mwingine"Amesema waziri Bashe.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa simiyu Dr YAHAYA NAWANDA amesema kwa mkoa wa simiyu kwa msimu wa 2022/2023 chakula ni toshelevu kwani mkoa umezalisha zaidi tano laki tano na themanini na nane elfu ya mazao ya chakula huku kukiwa na ziada ya tani elfu themanini na nane .
Pia Dr YAHAYA NAWANDA amesema kupitia maonyesho hayo wananchi wamepata mafunzo baada ya kutembelea mabanda pia wamekumbushwa namna ya kutumia vyakula vya asili vinavyopatikana Katika mkoa wa simiyu Ili kuimarisha lishe na kupunguza tatizo la udumavu na utapiamlo kwa watoto.
Maonyesho haya ya siku ya chakula duniani 2022 yanakaulimbiu isemayo uzalishaji Bora lishe Bora mazingira bora kwa watu wote habaki mtu nyuma.







0 Comments