Hayo yalisemwa Wilayani Kibaha na Grace Kalinga ambaye alimwakilisha Flaviana Msilu kutoka benki ya CRDB Bank PLC,Palm Beach Premier, wakati wa mahafali ya 15 ya shule ya Msingi Mwanalugali.
Kalinga alisema alisema kuwa wazazi waliowekeza kwa ajili ya watoto wao imewapunguzia mzigo wazazi ambapo bila kuweka akiba inakuwa changamoto kupata fedha kwa ajili ya kusomesha watoto.
Aidha wazazi wametakiwa kuwaendeleza watoto kielemu ili kufikia elimu ya juu badala ya kuwa kikwazo cha kuwakatisha masomo kutokana na sababu zao Jambo linalosababisha kukatisha ndoto za watoto.
Alisema kuwa Serikali imekuwa mkombozi mkubwa kwa Watanzania kusomesha kutoa elimu bure hadi kidato cha sita hivyo wazazi tusiwe chanzo cha kuharibu maisha ya watoto kwa kukatisha masomo yao bila sababu ya msingi.
Awali Mwalimu mkuu wa shule hiyo Hambari Mshana alisema kuwa Shule imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma na kufaulisha kwa asilimia 92 mwaka 2019, asilimia 100 mwaka 2020 na mwaka 2021 asilimia 95.
Kwa upande wake mhitimu Prisca Mussa alishauri kuwepo na upatikanaji wa chakula shuleni ili kupunguza utoro.
0 Comments