Naibu Waziri wa Wizara Ya Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli Tanzania TRC Mhandisi Masanja Kadogosa
Mkurugenzi Mkuu LATRA Habibu Suluhu
Na fatma Ally Matukio Daima APP Dar
Wananchi wametakiwa kutojihusisha kufanya shughuli zozote za kijamii(kibinaadam) ikiwemo biashara ndani ya hifadhi ya miundombinu ya reli Ili kulinda miundombinu hiyo na kupunguza ajali za mara kwa mara.
Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete wakati akifunga maadhimisho ya kilele wiki ya Usalama wa reli yaliofanyika jijini Dar es Salaam ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika kwa maadhimisho hayo nchini Tanzania.
Aidha, ameyapongeza mashirika mbalimbali yalioshirikiana na TRC ikiwemo TAZARA na LATRA kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu usalama wa reli katika maeneo mbalimbali, kwani usalama wa reli ni muhimu sana katika kupunguza ajali na kutunza miundombinu ya reli hivyo, wananchi wanatakiwa kukaa umbali wa mita 30 kwa mujibu wa sheria ya reli TRC na mita 50 kwa upande wa TAZARA.
"Wananchi wamehamasishwa kuwa makini wanapokuwa karibu na njia ya reli au wanapopita katika makutano ya reli na kuhakikisha shughuli za kijamii na kiuchumi hazifanyiki katika miundombinu ya reli shughuli za uhamasishaji katika mtandao wa reli TRC zimefanyika katika maeneo ya Bugurunu kwa mnyamani,Gongo la mboto,Karakata,Vingunguti,Pugu mnadani pamoja na Tabata mwananchi" amesema Mwakibete.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli Tanzania TRC Mhandisi Masanja Kadogosa amesema zoezi la kutoa elimu kuhusu usalama wa reli ni endelevu kwani wametekeleza kampeni za usalama wa reli katika vipindi tofauti, ambapo wametoa elimu katika maeneo tofauti Ili kuhakikisha watanzania wanata uwelewa juu ya Usalama wa reli.
Aidha, amesema kampeni hiyo wamewakumbusha wananchi kuwa usalama ni kitu Cha kwanza katika usafiri wa reli, hivyo wazingatie matumizi sahihi ya alama kwenye maeneo ya vivuko , hifadhi ya reli, stesheni na mradi ambapo wananchi hawatakiwi kufanya shughuli zozote za kibinaadam ndani ya miliki ya reli.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji TAZARA Mhandisi Bruno Chiganda ametoa wito kwa wananchi kuzingatia sheria ya reli na kueka umakini hasa kwa watu wanaoishi maeneo ambayo reli imepita kwa ajili ya usalama wao sababu treni inaenda haraka na inachelewa kusimama, huku akiipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa uwekezaji mkubwa katika Sekta ya reli.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu LATRA Habibu Suluhu, ametoa pongezi kwa TRC na TARAZA kwa kuendelea kutoa huduma bora za usafiri na kutoa elimu juu ya Usalama wa reli pamoja na kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika kutoa huduma kwa wateja ambao wanatumia reli .
"Lazima tuwatambue wale ambao tunawahudumia ambao ni wateja wetu abiria kuna Nchi jirani ambazo zinatumia bandari yetu na mizigo yao inasafirishwa kwa njia ya reli pia kuna wafanyabishara ambao mizigo yao inasafirishwa kwa njia ya reli hao wote ni wateja" amesema Suluhu.
0 Comments