Header Ads Widget

MUMTAAZ ENGLISH DAY PRIMARY SCHOOL KUANZISHA DARASA LA TEHAMA

 

Mumtaaz English Day & Primary School iliyopo eneo la Buhongwa Wilayani Nyamagana mkoani Mwanza imefanya Mahafali ya tano ya Darasa la V11 na ya Saba ya Wahitimu wa awali


Mumtaaz English Day & Primary School imefanya Mahafali ya tano ya Darasa la V11 na ya Saba ya Wahitimu wa awali huku Mwalimu mkuu wa shule hiyo Deogratius Makoko akisema, wahitimu wa shule ya awali na msingi waliandaliwa vizuri kwa ajili ya kuingia darasa la kwanza na kidato cha kwanza.


Mkuu wa Mumtaaz English Day & Boarding Pre & Primary School amesema, wanatarajia kufanya vizuri zaidi kitaaluma ili shule iendelee kuwa ya mfano huku akisema wanatajia mwezi january kuanza rasmi darasa la teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA.


Aidha Makoko amesema wamekuwa wakikumbana na changamoto kadhaa ikiwemo baadhi ya wazazi wa wanafunzi kushindwa kulipa ada za wanafunzi kwa wakati na hivyo kusababisha usumbufu kwa namna moja ama nyingine katika uendeshaji wa shule hiyo.


Pia akasema, matarajio ya shule hiyo ni kuwa  wanafunzi wa awali ya pili wanaohitimu masomo ya awali, watarudi mwakani wote na kuendelea na elimu ya msingi kutokana na elimu bora inayotolewa na walimu bora walionao.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI