Na Frederick Siwale- Matukio daima media .Makambako.
WANAFUNZI wenye mahitaji maalumu katika Halmashauri ya Mji Makambako Mkoani Njombe ,watazamwa upya kwa kupewa kipaumbele cha kupatiwa elimu sawa na wasio na uhitaji huo .
Haya yamebainishwa wakati wa mapokezi ya Wanafunzi wa kike wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Idofi iliyopo kata ya Mlowa nje kidogo ya Mji wa Makambako.
Mapokezi hayo yamefanywa kufuatia ujenzi wa bweni jipya ambalo limejengwa mtaa wa Idofi lenye thamani ya zaidi Milioni 94 ,ambapo hadi kufikia oktoba 14 ,2022 tayari Wanafunzi wa kike 20 walikuwa wamekwisha pokelewa kutoka katika mitaa na vijiji mbali mbali katika Halmashauri ya Mji Makambako.
Akizungumza katika hafla fupi ya kuwapokea Wanafunzi hao afisa elimu maalumu Halmashauri ya Mji Makambako Bi.Exavelia Mtega ,alisema bweni hilo limejengwa kwa ajili ya kuwapokea Wanafunzi wenye mahitaji maalumu kutoka sehemu mbali mbali Nchini na kuwataka Wazazi kuwafichua Watoto wenye mahitaji maalumu badala ya kuwafungia ndani.
Upande wake Mwenyekiti wa taasisi ya UMOJA WA AMANI KWANZA (U.A.K) Bw.Lusungu Kaduma ameitaka Jamii kuachana na mitazamo hasi kuhusiana na Watoto wenye ulemavu na mahitaji maalumu kwa kuhakikisha wanapatiwa haki ya msingi ikiwepo kulindwa, kutunzwa na elumu kwa kupeleka shule badala ya kuwa nyanyapaa na kuwaficha majumbani.
"Wanachama wa Umoja wa amani kwanza tumefika hapa shuleni kwa malengo mahususi ikiwa ni pamoja na kuipatia jamii elimu ya utunzaji amani ili kuepusha uovu na vitendo vya vinavyoweza kuashiria uvunjifu wa amani"Alisema Bw.Kaduma.
Bweni hilo lenye uwezo wa kupokea zaidi ya Watoto 80 limejengwa na Serikali kuu ambayo imetoa milioni 80 huku Halmashauri ya Mji Makambako ikichangia zaidi ya milioni 14 katika ujenzi huo.










0 Comments