Header Ads Widget

RAIS SAMIA AKUTANA NA MAMA MZAZI WA HAYATI MAGUFULI

 


Rais Samia Suluhu Hassan amemtembelea Suzana Magufuli, mama mzazi wa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli, nyumbani kwake huko Chato mkoani Geita wakati wa ziara yake.Rais Samia pia ametembelea pia kaburi la Hayati Magufuli ambaye alifariki dunia Machi 17, 2021 jijini Dar es Salaam na kufanya dua kumwombea mtangulizi wake.

Rais Samia ameanza ziara yake mkoani Geita leo Oktoba 15, 2022 akitokea mkoani Kagera alikokwenda kuhitimisha mbio za Mwenge kitaifa pamoja na kushiriki ibada maalumu ya kumbukumbu ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI