Header Ads Widget

WALIMU WA PAMBAZUKO - SONGEA WAISHUKURU KAMPUNI YA BARAKI TWIST KWA MCHANGO WA FEDHA SH.1,200,000=



 Na Amon Mtega, Songea.

WALIMU wa Shule ya Msingi Pambazuko kata ya Tanga Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wameishukuru kampuni ya Baraki Twist Limited tawi la Songea inayojishughulisha na utoaji wa mikopo kwa  kuwachagia fedha sh.Milioni moja na Laki moja (sh.1,100,000=) kwa ajili ya kutengenezea meza 10 na viti pamoja na mipira miwili yenye thamani ya sh.Laki moja(sh .100,000=)na kufanya jumla ya fedha sh.Milioni Moja na Laki mbili (sh.1,200,000=).


Akishukuru mkuu wa shule hiyo Deogratius Komba kwa niaba ya walimu wenzake pamoja na wajumbe wa kamati ya shule kwenye  mahafali ya darasa la saba ya 19 ambapo mgeni rasmi imekuwa kampuni ya Baraki Twist amesema kuwa msaada waliopatiwa ni mkubwa jambo ambalo hawakutegemea.


Mwalimu Komba ambaye amepokea fedha hizo pamoja na mipira miwili ya  miguu ambayo watachezea wanafunzi wa shule hiyo amesema kuwa kulikuwa na changamoto kubwa ya upungufu wa meza za walimu pamoja na viti kwa sasa changamoto hiyo inaenda kupungua.


Amesema kuwa ilifikia wakati baadhi ya walimu wamekuwa wakikaa kwenye madawati kisha kusahisha madaftari au mitihani ya wanafunzi jambo ambalo limekuwa likiwapa shida walimu.


Kwa upande wake mgeni rasmi James Mhere ambaye ni mmoja wa Wafanyakazi wa kampuni ya Baraki Twist akizungumza kwa niaba ya kampuni hiyo amesema kuwa wametoa fedha hizo na mipira miwili ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya Elimu.


 Mgeni rasmi huyo licha ya kutoa mchango wa fedha hizo lakini bado ameongoza harambee kwa Wazazi wa mtaa huo ili  kuchangia ununuzi wa baadhi ya vifaa vinavyohitajika shuleni hapo .


 Naye shekh wa mtaa wa Pambazuko Issa Mohamed amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa shule hiyo Wananchi ndiyo waliokuwa wakijitolea nguvu zao ila leo hawaamini kupatiwa msaada mkubwa kama huo ambao umewaletea chachu katika Shule hiyo.

Mkuu wa Shule Deogratius Komba akipokea Fedha kutoka Mwakilishi wa Kampuni ya Baraki Twist James Mhere
Mwakilishi wa Kampuni ya Baraki Twist James Mhere akikabidhi mipira kwa Mwanafunzi wa shule hiyo.
Mwakilishi wa Kampuni ya Baraki Twist James Mhere akizungumza shuleni hapo
Mwalimu Mkuu Deogratius Komba akishukuru kwa mchango huo toka Kampuni ya Baraki Twist


Mzazi akiishukuru Kampuni ya Baraki Twist kwa mchango huo shuleni hapo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI