Na fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam.
Vyama 14 vya siasa visivyo na wawakilishi Bungeni vimeshangazwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kuiponda ripoti ya kikosi kazi iliyotolewa October 21 kwa Rais waJamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kudai kuwa ripoti hiyo ni ya ovyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Chama cha ADC, ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Baraza la vyama vya siasa Doyo Hassan Doyo amesema kuwa kauli iliyotolewa na CHADEMA imejaa ubinafsi , choyo na wivu mkubwa kuona Tanzania inaweza ikawa katika maridhiano huku wao wakiwa nje ya mchakato huo.
"Kwa nini tunasema CHADEMA imeonyesha Ubinafsi wa hali ya juu, kwa kuwa ni wazi tunafahamu baada ya wadau wa siasa kukutana jijini Dodoma Chama hicho kilisusia vikao hivyo wakituhumu kuwa hawawezi kukaa meza moja na msajili wa vyama vya siasa kutafuta muafaka, bahati nzuri wadau wengine walishiriki na kuja na maazimio ambayo pia CHADEMA waliyapinga wakiwa nje ya mashauriano"amesema Doyo.
Hata hivyo, ameongeza kuwa licha ya kupinga kikao na maadhimio yaliyotolewa lakini pia chama hicho walidai nafasi ya kuonana na Rais Samia wakijinasibu kuwa wana jambo la kipekee la kumueleza ambapo waliipata nafasi hiyo kupitia kwa mwenyekiti wao wa Chama Taifa Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti wao bara ndugu Tundu Lissu.
Aidha, amesema taarifa ya kikosi kazi ndiyo kwanza imewasilishwa Oct 21 mwezi huu kwa Rais Samia na bado haijawekwa hadharani, hivyo walitarajia chama kinaacho jinasibu juu ya ukubwa wake kisingefanya mambo kama taasisi isiyokuwa na watu makini, na kuwataka waipitie au wasubiri iwekwe hadharani ndiyo waikosoe badala ya kukimbilia taarifa za juu juu.
"Kama mnavyofahamu juzi mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,alipokea ripoti ya kikosi kazi kilichoundwa mapema mwaka huu kwa ajili ya kutafuta muafaka wa kitaifa na kutoka katika mkwamo tuliokuwa nao awali hususan mkwamo wa kisiasa"amesema Doyo
Ameongeza"Kikosi Kazi kiliundwa baada ya Mkutano wa wadau wa Demokrasia Dodoma Mwezi Desemba 2021. Rais alichukua Wajibu wa kikosi Kazi kufuatia Pendekezo la kuundwa kwa Timu hiyo kuchakata maoni ya Wadau yaliyotolewa katika Mkutano ule. Mkutano ule ulikuwa ni chachu ya kuleta Majadiliano Nchini ili kujenga mwafaka wa Kitaifa"
Amesema kuwa, kwa miaka sita walikua na hali ngumu kisiasa, lakini Tangu Rais Samia ameingia madarakani, miongoni mwa mambo ya awali aliyoyapa kipaumbele ni kutafuta suluhu ya kitaifa kwa kufanya vikao na wadau mbali mbali wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa kabla ya kuundwa kwa kikosi kazi kilichokabidhi kazi yake juzi.
Aidha, amesema wao kama wadau wa maridhiano na wajenzi wa Taifa lenye umoja wamepokea mapendekezo yaliyotolewa na Kikosi Kazi, hususani katika eneo la kuviwezesha vyama kufanya kazi zao kwa mgawanyo wa ruzuku, hivyo wanamtaka Msajili wa vyama atekeleze agizo la Rais na Taarifa kuwa wazi kwa umma,katika yale mapendekezo yote yaliyo chini ya ofisi yake.






0 Comments