Header Ads Widget

UONGOZI WA SHULE ZA ST. MATHEWS WAELEZEA MFUMO WA ELIMU WANAYOTOA

 


Uongozi wa shule za St. Mathews katika mikoa ya Dar es salaam, Pwani na iringa umesema unatoa elimu ya darasani na elimu ya nje ya darasa kwa kuwapa wanafunzi ujuzi wa fani mbalimbali ili waweze kujiajiri na kujipatia kipato baada ya kuhitimu masomo yao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shule hizo za St. Mathews Peter Tadeus Mutembei wakati akitoa taarifa kwenye mahafali ya 19 ya shule ya Sekondari ya St. Mark's iliyopo Mbagala jijini Dar es salaam.

Peter amesema uongozi wa shule hizo umedhamiria kutoa huduma kwa kutoa elimu kwa Watoto wa kitanzania nchini na sio kufanyabiashara kwa lengo la kuchochea ukuaji wa maendeleo ya elimu nchini kwa kuchochea taaluma Bora kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kutoa stadi za kazi kwa wanafunzi kuwajengea uwezo wa kuajiriwa na kujiajiri katika maisha yao.

"Elimu tunayotoa katika shule zetu tunazingatia katika mambo makuu matatu ya elimu, malezi na usalama ili watoto wapate elimu Bora kwa kuzingatia taaluma bora ndio maana wanafaulu vizuri mitihani yao kwa kuhakikisha tunatoa elimu Bora darasani na elimu ya nje ya darasa kwa kuwapa ujuzi wa fani mbalimbali ikiwemo ufugaji, kilimo, mapishi na ufinyanzi" 

"Kwani mtoto anapotoka shule anakwenda kuishi kwenye jamii zetu mtaani ambako anahitaji fani mbalimbali za stadi za kazi na ujuzi wa fani mbalimbali kwani elimu ya darasani pekee haitatosha kumsaidia Mwanafunzi katika maisha" alisema Peter.

"Mwanafunzi anatakiwa awe na ujuzi na maarifa ya kutumia ile elimu aliyopata darasani katika maisha yake ya kila siku katika jamii hivyo katika shule zetu tunawafundisha ili akaitimie elimu yetu.katika kuendeleza maisha yake ya kila siku" alisema Peter.

Alisema katika elimu ya maisha wanawafundisha ujasiriamali ambao ni kutengeneza bidhaa mbalimbali ambazo zitawaongezea kipato kwa kutengeneza bidhaa na kuzibadilisha hizo bidhaa kupata fedha.

"Yaani tunawajengea uwezo wa kuweza kutambua changamoto na kutumia changamoto zilizopo katika jamii zao kwa kuzitatua ili wapate fedha" alisema.

"Kila Mwanafunzi hapa anafundishwa kutengeneza Sabuni za maji, dawa za kusafishia nyumba, kutengeneza mafuta ya mgando, ufugaji wa kuku, ufugaji wa samaki mapishi ili hata wakihitimu masomo yao wakaweze kujipatia kipato kwa njia yoyote ya ujasiriamali" alifafanua.

Alisema Kati yao wapo wanafunzi wanatamani kusoma lakini kwa sababu mbalimbali hukosa ada na mahitaji ya shule hivyo uongozi wa shule hizo huwasaidia Wazazi na walezi kulipa ada.

Aidha amempongeza Mheshimiwa Rais Samia kwa nguvu kubwa anayotumia katika kuhakikisha maendeleo na mafanikio katika sekta ya elimu nchini.

"Kwanza nimpongeze kwa kuboresha elimu yetu, kwa kuboresha shule yaani mazingira ya kujifunzia yamekuwa Bora sana na kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu bure kabisa kwa kuwapunguzia Wazazi na walezi mzigo wa kuwasomesha watoto wao" 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI