Hayo yamebainishwa na Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Lazaro Kilahala mwishoni
mwa wiki hii wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Yadi ya Songoro
Kigamboni jijini Dar es Salaam ambapo kivuko hicho kinaendelea kufanyiwa ukarabati.
‘’Tumefanya ukaguzi wa mwisho
takribani mwezi mmoja uliopita, kikubwa kilichokuwa kinasubiriwa ilikuwa ni
vifaa, kwa sababu ile kazi sehemu kubwa ilikuwa ni kufunga vifaa vipya vya
injini, gia boksi, na mifumo mipya ya injini, kwa hiyo zile kazi ambazo zilikuwa
zinaweza kufanyika kabla ya vifaa hivyo ilikuwa zaidi ya asilimia themanini na zote
zilifanyika ikiwemo kazi za kuondoa
vipande vya bati ambavyo vimeharibika na kupiga rangi upya. Alisema Mtendaji
Mkuu.
Awali Mwakilishi wa kampuni ya
Songoro Marine wanaofanya ukarabati wa kivuko hicho Hamad Aweso akizungumza na
waandishi wa habari amesema ukarabati wa kivuko hicho umefikia hatua nzuri na
amebainisha kuwa kuna vifaa ambavyo vilichelewa kufika kwa wakati zikiwemo
injini za kivuko hicho na kwa sasa vifaa hivyo vimeshafika hivyo kazi iliyobaki
ni kuvifunga ili kivuko kiweze kurejea kutoa huduma. ‘’kwa sasa hivi zoezi linaloendelea ni la kufunga hizi injini
na kwa hali inavyoendelea tunategemea mwisho wa mwezi wa kumi na moja zoezi
zima litakuwa limekamilika na chombo kitakuwa kimekwishaingizwa majini, alimaliza mkandarasi huyo.
Kivuko cha MV. KAZI kina uwezo wa
kubeba abiria 800 na magari 22 sawa na tani 170 na tangia kuondolewa kwa kivuko
hicho, eneo la Magogoni Kigamboni limebakia na vivuko viwili ambavyo vinatoa
huduma kikiwemo kivuko cha MV. MAGOGONI na MV. KIGAMBONI ambavyo kwa sasa
vinasaidiana na vivuko viwili kutoka kampuni ya Azam Marine kutoa huduma eneo
hilo.
0 Comments