Header Ads Widget

IDADI YA WATANZANIA KULINGANA NA MATOKEO YA SENSA YA WATU YA MWAKA 2022 NI MILIONI 61.74

 

NA HAMIDA RAMADHAN DODOMA

RAIS Samia Suluhu Hassan ametangaza matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika Mwezi Agosti mwaka huu 2022 nakusema  hadi sasa Tanzania ina idadi ya watu milioni 61.74, kati yao wanawake ni milioni 31.6 sawa na asilimia 51 na wanaume milioni 30.53 sawa na asilimia 49 ya watu wote na kati ya hao Watanzania milioni 59.8 wako Tanzania Bara na milioni 1.8 wako Zanzibar.


Aidha kwa upande wa Mikoa, Rais Samia amesema Mkoa wa Dar es Salaam ndio unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu nchini ambao ni milioni 5.3 sawa na asilimia 8.7na kufuatiwa na Mwanza ambao una watu milioni 3.6 sawa na asilimia sita na kufafanua kwamba katika kipindi cha miaka 10 kuna ongezeko la watu milioni 16.8 sawa na asilimia 3.2.


Rais Samia ametangaza idadi hiyo ya watu Jijini Dodoma Katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, ambapo alisema kuwa kati ya Idadi hiyo ya watu Tanzania Bara ni watu 59,851,357 na Zanzibar ni watu 1,889,773.


Alifafanua kuwa kati ya idadi hiyo ya watu Wanawake ni Milion 31,688790 sawa na asilimia 51 na wanaume ni milioni 30,53130 sawa na asilimia 49


"Idadi hii ni Ongezeko la watu zaidi ya milioni 19 ukilinganisha na sensa ya miaka kumi iliyopita yaani 2012 ambapo kipindi hicho idadi ilikuwa milioni 44,928,923.


Pamoja na hayo Rais Samia alitaja Mikoa iliyoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu ni Mkoa wa kwanza ni Dar-es-salaam ina watu milioni 5,383,728 na Mwanza ina watu milioni 3,699,872 hii ni kwa upande wa Tanzania Bara.


Na kwa upande wa Zanzibar Mkoa unaoongoza ni Mjini Magharibi yenye idadi ya watu zaidi ya laki nane (800000)


Rais Samia amewaagiza viongozi katika ngazi zote kutumia muongozo aliyouzindua leo kwa ajili ya kuzidi kuwaletea maendeleo watanzania.


"Ni wajibu wa kila mdau kuanzia sekta binafsi na sekta za umma kutumia muongozo huu kuwahudumia wananchi kwa sababu tayari tuna idadi ya watu tunaotakiwa kuwahudumia katika kila nyanja iwe ni huduma ya Afya,elimu na kwinginepo,"Alisema Rais


Kwa Upande wake Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ally Mwinyi alisema kuwa Mwongozo huo wa matumizi ya Sensa utaongeza wigo wa matumizi ya sensa katika kuandaaa matumizi ya maendeleo na kuahidi kutumia mwongozo huo katika kupanga Mipango ya maendeleo.


Naye Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar na Mwenyekiti mwenza wa Sensa,Hemed Suleiman Abdulah alisema kuwa Sensa hiyo itawasaidia katika masuala ya Kitaifa na Kimataifa na Wataalam kuzifanyia uchambuzi takwimu hizo za sesnsa.


Kwa Upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa Kitaifa nae ameahidi kutumia takwimu hizo katika kupanga Mipango ya maendeleo.


Awali Mtakwimu Mkuu wa Serikali,Dkt,Albina Chuwa alioyaomba mabenki kutokuwa na masharti magumu pale wafanyabiashara wanapoenda kukopa kutokana na kuwa na kanzi data yenye taarifa za wafanyabiashara hao,kazi iliyobaki ni uchambuzi wa kina.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI