Header Ads Widget

TARI KIBAHA YAPONGEZWA KWA UTAFITI WA MBEGU BORA

 





Na junior Mwemezi Kilombero Morogoro


Mkuu wa mkoa wa Morogoro mheshimiwa Fatma Mwassa ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Kilimo kituo cha Kibaha kutokana na Utafiti wa mbegu bora wa zao la miwa.


Mheshimiwa Mwassa alitoa pongezi hizo mara baada ya kutembelea vipando vya TARI kibaha katika viwanja vya Them vilivyopo bonde la mto Kilombero mkoani Morogoro.


Alisema TARI kibaha pamoja na Utafiti nzuri wa mbegu inatakiwa kuzalisha mbegu hizo kwa wingi ili ziweze kuwafikia wakulima na hivyo kuongeza uzalishaji.



"Tunataka kuona sasa mnazalishaji mbegu nyingi bora na kuwafikia wakulima,hayo ndiyo maelekezo ya waziri,alisema mheshimiwa mkuu wa mkoa wakati akisoma risala ya waziri wa Kilimo kwa wakulima waliohudhuria maonesho hayo ya siku ya wakulima wa miwa.


Akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa,mratibu wa zao la miwa nchini bi Minza Masunga alisema uzalishaji wa mbegu bora kwa wakulima unaendelea.


"Tumejipanga kuhakikisha tunazalisha mbegu bora za kutosha na bahati nzuri Utafiti tumeshafanya na kupata mbegu bora ambazo zinawafaa wakulima wetu,kazi kubwa tuliyonayo kwa sasa ni uzalishaji wa mbegu hizo,alisema bi Masunga.



Meneja wa TARI kibaha Dkt Nessie Luambano aliwaambia waandishi wa habari kwamba kituo chake kinatekeleza maagizo yote ya serikali katika uzalishaji wa mbegu bora.


"Tumejipanga vizuri kuhakikisha wakulima wetu wanapata mbegu bora za miwa,niwatoe hofu wananchi kazi hiyo tunaifanya kwa weledi mkubwa,alisema dkt Luambano.



Taasisi ya Utafiti wa Kilimo kituo cha Kibaha kwa kushirikiana na wadau wengine nchini huandaa siku ya wakulima wa miwa ili kutoa fursa kwa wakulima kujionea teknolojia mbalimbali za Kilimo bora cha miwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI