Header Ads Widget

BARUA YA WAZI KWA RAIS

 


Tunamshukuru Sana Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Tanzania kwa uamuzi wa kuwalipa watumishi walioshutumiwa na vyeti.

Pamoja na shukrani hizi kubwa kwake lakini tuna ombi kubwa kwake.


 Na Kama alivyokuwa amesema Mei mosi 2022 kwamba kwa wale ambao wametumikia miaka mingi na wamekaribia kustaafu Basi walipwe mafao yao yote Basi angefanya hivyo. Kulipwa 5% alivyokuwa anakatwa kwenye mshahara wake tu Ni kitu kidogo Sana sidhani Kama zinafika hata milioni 5 hazifiki.

 Kwa moyo wa mama yetu, moyo wa huruma, moyo wa umama, moyo wa huruma aendelee kuwahurumia watumishi hawa, awahurumie Sana Sana walioitumikia Taifa hili katika wakati mgumu Sana mfano Kama watendaji wa kata wametumikia kazi wengine toka mwaka 1993 Ni zaidi ya miaka 26 Hadi 29 leo aje apewe m.3 au 4 hivi kweli! Kwa kazi ngumu Kama hiyo. Mama yetu mpendwa, mama yetu mwenye huruma na Upendo, tusaidie/ wasaidie, wahurumie, Mungu atakulipa mama! Uwalipe hawa fedha zao na mafao yao na tayari wamesha staafu wengine jamani. 

 Ni matarajio yangu waandishi wa habari* mtaendelea kumsihi mama, Rais wetu mpendwa alione hili na kutusaidia.

Mama yetu Mhe  Samia Suluhu Hassan tunakuomba Sana utuhurumie. Wengine tumezeekea huko na Sasa hatuna kitu. Tukifanyakazi kwa moyo wote Tena katika wakati mgumu Sana na mishahara yetu ilikuwa midogo mno. Tuonee huruma, TUHURUMIE utulipe mafao yote tupumzike na Mungu akubariki.

 Matukio daima Soma vizuri hii Kisha paza sauti tusaidie. Mwambie na Mkuu wa KKKT atusaidie kutufikishia kilio hiki

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI