Header Ads Widget

TAKUKURU NJOMBE KUFUATILIA KIASI CHA TSH BILIONI 555 ZA MIRADI

 


Na Gabriel Kilamlya matukio DaimaAPP NJOMBE


Wakati serikali kupitia wizara ya afya ikitenga kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 555 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo,Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru mkoa wa Njombe imesema itahakikisha inafanya ufuatiliaji wa karibu wa miradi yote inayotekelezwa ili kuwasaidia wananchi. 


Katika utambulisho wa mradi wa mfumo wa ufuatiliaji wa matumizi ya umma[PETS] ili kuboresha huduma za afya unaokwenda kutekelezwa na  Asasi isiyo ya kiserikali ya Highlands hope Umbrela[HHU] katika vijiji vya kata ya kifanya Halamshauri ya mji wa Njombe,mkuu wa dawati la uzuiaji rushwa  TAKUKURU mkoa wa Njombe Akohek Mbapila  anasema mradi huo utatekeleza majukumu ambayo wao wanayafanyia kazi wakati wote hivyo  watakuwa bega kwa bega katika zoezi la ufuatiliaji.



Mratibu wa mradi huo  toka HHU Bwana Kelvin Mwinuka amesema lengo kuu la mradi ni kuongeza dhana ya uwazi na uwajibikaji katika mapato na matumizi kwenye sekta ya afya ili kuboresha utoaji na upatikanaji wa huduma za afya huku kaimu mkurugenzi wa shirika hilo Bi.Lilian Barnabasi akieleza namna wanavyotekeleza miradi mbalimbali  na kuyahudumia makundi maalum yakiwemo ya wazee,wajane na wagane,watoto na watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.


Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya mji wa Njombe Enembora Lema amekiri kuupokea vyema mradi huo huku kaimu mganga mkuu Lusato Kajanja akisema ni fursa kwao katika kuhakikisha miradi ya afya inayotekelezwa inafuatiliwa kwa maslahi mapana ya taifa.


Kwa niaba ya mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Njombe diwani wa viti maalum jimbo la Njombe mjini Angela Mwangeni ambaye alikuwa mgeni wa heshima katika utambulisho wa mradi huo amesema serikali ipo bega kwa bega na asasi za kiraia katika kutekeleza miradi mbalimbali kwani zimekuwa zikiisaidia kupunguza baadhi ya majukumu yake.


Katika mradi huu wa ufuatiliaji mapato na matumizi ya umma katika sekta ya afya,shirika hilo limepata ufadhili wa zaidi ya shilingi milioni 50 zitakazotekeleza mradi huo katika kipindi cha miaka miwili katika kata ya kifanya.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI