Header Ads Widget

ACT WAZALENDO KUISIMAMIA SERIKALI MAJIMBONI.

 

Chama cha ACT Wazalendo kimebainisha kuwa kitaweka utaratibu wa kufuatilia na kusimamia uwajibikaji wa Serikali kwenye majimbo yote Nchini. 


Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu akizungumza na wanachama na wapenzi wa ACT Wazalendo katika Kata ya Ligunga Jimbo la Tunduru Kaskazini Mkoani Ruvuma.


"Tunduru sitowaacha. Tunafahamu kuwa madiwani na wabunge hawawajibiki kushughulikia kero zenu. Nimezunguka Tunduru Kusini na Kaskazini, kote kumejaa kero ambazo zinapaswa kufuatiliwa. Inasikitisha kuwa wabunge wa hapa wameamua kuwa mabubu Bungeni"-alisema Ado.



"Mimi na Mtutura (aliyekuwa Mgombea Jimbo la Tunduru Kusini) tutakuwa Wabunge wa Nje ya Bunge. Tutapaza sauti dhidi ya mauaji yanayofanywa na tembo, stakabadhi ghalani, uingizwaji holela wa Ng'ombe na kupigania huduma nzuri za kijamii kwa Wanatunduru"-alisisitiza Ndugu Ado na kuongeza:


"Utaratibu huu utakuwa kwa majimbo yote Nchini. Tutaweka utaratibu wa kuwa na sauti Nje ya Bunge ya kuwasemea wananchi. Lengo letu ni kuwa sauti mbadala ya uhakika kwa wananchi"-alihitimisha Ndugu Ado.


Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo anaendelea na ziara yake ya wiki moja ya kuimarisha Chama kwenye majimbo ya Tandahimba, Tunduru Kusini na Tunduru Kaskazini iliyoanza tarehe 30 Oktoba na kutarajiwa kumalizika tarehe 06 Oktoba 2022.


Janeth Joel Rithe, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, ACT Wazalendo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI