Header Ads Widget

RAIS SAMIA ASAIDIA WENYE MAHITAJI, TAASISI ZA DINI KIGOMA

 


Fadhili Abdallah,Kigoma


RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa msaada wa vitu mbalimbali kwenye vituo vinane vya watu wenye mahitaji maalum na taasisi za dini ikiwa ni siku chache baada ya ziara yake ya kiserikali ya siku tatu mkoani Kigoma.


Misaada hiyo iliyotolewa na Rais Samia ilikabidhiwa kwa walengwa na Mkuu wa mkoa Kigoma, Thobias Andengenye  ambaye pamoja  na misaada hiyo aliwasilisha pia salamu za kiongozi huyo kwa walengwa.


Miongoni mwa maeneo yalipokea msaada huo ni pamoja na Msikiti wa Muumini uliopo Ujiji mjini Kigoma ambapo kwa niaba ya waumini wa msikiti huo Shekhe wa mkoa Kigoma,Hassan kiburwa alipokea juzuu za Quran 300, Tasbihi 300,Kofia,mikeka na miswala 30.




Vituo vingine vilivyofaidika na misaada hiyo ya Rais Samia ni Pamoja na msikiti wa Ijumaa vituo viwili vya kulelea watoto vya Sanganigwa vilivyopo mjini Kigoma vinavyosimamiwa na kanisa katoliki jimbo la Kigoma, kituo cha kulea watoto watoto kilichopo kwenye shule ya Kiislam ya Juve Gungu mjini Kigoma.


Vingine ni kituo cha kusaidia na kulea watoto cha MWOCACHI, kituo cha kusaidia wazee (SILABU) vilivyopo Kibirizi mjini Kigoma, kituo cha kulelea watoto cha Matyazo Kigoma Vijijini na kituo cha kulea watoto Yatima cha Bangwe.


Miongoni mwa misaada iliyotolewa ni pamoja na Vitabu vya dini (Quran), tasbihi, misala, madaftari, kalamu ,vikombe na chakula kwa vituo vya watoto yatima na makazi ya wazee wasiojiweza.




Akizungumza kwenye maeneo tofauti wakati akikabidhi misaada hiyo kwa naiaba ya Rais Samia Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa Rais Samia amefarijika kwa mapokezi makubwa na ukarimu wa wananchi wa mkoa Kigoma hivyo ameona ana kila sababu ya kusaidia makundi mbalimbali ikiwemo yatima na wazee wasiojiweza.


Rais Samia katika ujumbe wake kwa makundi hayo alisema kuwa serikali yake itaendelea kusaidia mkoa Kigoma uweze kupiga hatua za maendeleo kwa haraka .


Kwa upande wake Shekhe Mkuu wa Mkoa Kigoma, Hassan Kiburwa alishukuru kwa msaada uliotolewa na Rais Samia na kueleza kuwa ni namna gani ameonyesha kujali watu wa kada mbalimbali kwa kuangalia utu wao kama Watanzania bila kujali msingi wa dini wala itikadi zao.


Msimamizi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Sanganishwa kinachoendeshwa na kanisa katoliki jimbo la Kigoma, Sister Leonida Aloyce akizungumza baada ya kupokea msaada wa madaftari,chakula, vikombe na vifaa vingine alimshukuru Rais Samia kwa wema wake na kuwajali wenye mahitaji. 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI