Header Ads Widget

BILLIONI 9 ZATUMIKA KWENYE MIRADI CHUO CHA MIPANGO NA MAENDELEO VIJIJINI.

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma

JUMLA ya Shilingi bilioni 9 zimetumika kugharamia utekelezaji wa miradi ya uendelezaji na utunzaji wa miundombinu ya Chuo Cha Maendeleo Vijijini Mipango ambapo Shilingi bilioni 5 zimetumika katika ujenzi wa kumbi Tatu za mihadhara na mabweni mawili ya wanafunzi wa kike


Hayo yalisemwa leo Jijini hapa na Mkuu wa Chuo  Profesa Hozen Mayaya Wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekekezaji wa vipaumbele vya Taasisi kwa mwaka 2022/2023.

Alisema kati ya Shilingi bilioni 9, Shilingi bilioni 4 ambazo ni mapato ya ndani zimetumika kutekeleza miradi katika Kituo cha Mafunzo kilichopo Mwanza ikiwemo ujenzi wa mgahawa, jengo la utawala, maktaba na kununua ardhi kwa ajili ya upanuzi wa chuo.


Alisema katika mwaka wa masomo 2021/22, chuo kimeendesha program za muda mrefu 31. Aidha, mpaka kufikia Juni 2022, washiriki 31 wa nje wamepatiwa mafunzo ya muda mfupi.


"Kwa mwaka 2021/22, chuo kimesajili jumla ya wanafunzi 14,461. Aidha, jumla ya Wahitimu 8,200 wamehitimu mwezi Disemba, 2021 ," Alisema Prof Mayaya


Aidha Alisema katika mwaka wa fedha 2021/22, chuo kiliwezesha wahadhiri wake kufanya tafiti Saba zinazolenga kutatua matatizo ya kijamii, kiuchumi na kuchangia kuandaa sera na miongozo mbalimbali ya kitaifa.


"Chuo kinatekeleza mradi wa "Higher Education for Economic Transformation" ambao umetenga Shilingi bilioni 6.85 kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufundishia, kujifunzia kwa kujenga jengo moja la taaluma, kuboresha mitaala na kuwajengea uwezo Wahadhiri," Alisema Prof Mayaya



VIPAUMBELE VYA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA CHUO KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23


Vipaumbele ni pamoja na kuongeza udahili na usajili wa wanafunzi kutoka 14,417 mpaka kufikia wanafunzi 16,663 na kuendelea kufanya tafiti na kutoa huduma za ushauri na uelekezi kwa kufanya tafiti saba na kuandika kitabu kuhusu maendeleo vijijini.


Kuendelea kupitia mitaala ya mafunzo ya muda mrefu na kuandaa mitaala ya kozi mpya na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kujenga miundombinu ya kufundishia.


Alisema Kuajiri watumishi wapya, kulipa stahili mbalimbali, kupandisha vyeo watumishi waliokidhi vigezo pamoja na kuboresha huduma za ustawi na kuongeza uwezo wa kielimu na kiutendaji kwa watumishi 396.


Alisema  Kipaumbele kingine ni ufanya ukarabati mkubwa na mdogo wa nyumba 13 za watumishi, kulipa madeni ya watumishi na watoa huduma, kutekeleza shughuli ambazo hazikutekelezwa katika Mpango Mkakati wa mwaka 2016/17-2020/21 pamoja na uendelezaji wa maeneo ya Miyuji Kaskazini, Chigongwe na Kiseke.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI