Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewaomba radhi Wakenya na Wana Afrika Mashariki kwa ujumla kufuatia Mtoto wake Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuandika kwenye mtandao Twitter kauli ambazo zililenga kuvuruga uhusiano wa kidiplomasia ikiwemo kauli ya kutaka kuiteka Nairobi na kumtaka Kenyatta agombee muhula wa tatu kinyume na Katiba.
Museveni amesema haikuwa sahihi kwa Muhoozi ambaye alikuwa Kamanda wa Jeshi la Ardhini Uganda kabla ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo jana, kuandika alichokiandika na kusema ule haukuwa msimamo wa Serikali ya Uganda.
Museveni ametolea pia ufafanuzi kuhusu sababu za kumpandisha cheo Muhoozi kutoka kuwa Luteni Jenerali na kumpa Ujenerali licha ya kauli zake hizo ambapo amesema licha ya kosa lake hilo Muhoozi anayo mazuri mengi na mchango mkubwa alioutoa na anaoweza kuendelea kuutoa “Nimetumia formula ya kuoneshwa kutopendezwa na mabaya huku wakati huohuo nikimtia moyo Muhoozi kwa mazuri yake”
“Samahani sana Ndugu zetu Wakenya na Watu wa Uganda ambao mlikasirishwa na kauli za Muhoozi, mbali na ombi hili la wazi nimewasilisha pia samahani yangu nyingine ya siri kwa Rais wa Kenya, William Rutto”






0 Comments