Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema kuwa mtoto wake, Muhoozi Kainerugaba atakaa kando kwenye mtandao wa Twitter linapokuja suala la mijadala ya mambo ya Serikali.
Hiyo ni baada ya kuibuka mijadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu maandiko yenye utata ya Kainerugaba anayopostio kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter.
Jenerali Kainerugaba (48), mara nyingi amezua utata kutokana na maoni yake anayoweka kwenye Twitter ambapo hivi karibuni aliweka andiko la kumlaumu Rais mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa kutogombea muhula wa tatu wa uongozi wa nchi hiyo hali iliyosababisha baba yake kuingilia kati.
0 Comments