Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akimwakilisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan leo Jumapili tarehe 09 October, 2022, amejumuika na viongozi mbalimbali wa Jumuia ya Afrika Mashariki katika sherehe za kutimiza miaka 60 tangu Uganda ilipojipatia Uhuru kutoka kwa Waingereza.
Sherehe hizo zinafanyika katika uwanja wa sherehe wa Kololo ambazo zimepambwa kwa gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama vya Uganda zinazongozwa na Rais Yoweri Kaguta Museveni na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Uganda na wageni waalikwa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi zinazounda Jumuia ya Afrika Mashariki.
0 Comments