Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira amesema huenda angekuwa chawa wa Rais wa kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere kama angekuwa hai.
Mwalimu Nyerere alifariki dunia Oktoba 14, 1999 London, nchini Uingereza alipokuwa amekwenda kwa matibabu.
Wasira ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 14, 2022 kwenye kongamano la kuenzi maisha ya Mwalimu Nyerere lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine (Saut), Mwanza huku akisema angefanya hivyo kutokana na uzalendo aliyokuwa nao kiongozi huyo.
0 Comments