Teddy Kilanga ARUSHA
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uhandisi na Usanifu mitambo(Temdo) Prof. Frederick Kahimba amesema katika kukuza uchumi wa viwanda nchini wamefanikiwa kubuni teknolojia mbalimbali za kisasa ikiwemo mtambo wa kuchakata mihogo kwa muda mfupi lengo ni kupunguza gharama ya uagizaji nje ya nchi.
Akizungumza katika maonyesho ya sido kanda ya kaskazini,Prof.Kahimba alisema mtambo huo unachakata mihogo tani 12 na kuweza kupata tani tatu za unga siku hiyohiyo ikiwa lengo la kubuni mtambo huu ni kumrahisishia mzalishaji kuona tija katika uzalishaji wake.
Pia alisema taasisi yao wamesanifu na sasa wanatengeneza mitambo kwa ajili ya kutengeneza sukari kwa kiwango cha mjasiriamali mdogo na wa kati ambapo mitambo hiyo inauwezo wa kuchakata tani 200 za muwa wa sukari kwa siku nakutoa tani 20.
"Mtu yeyote akiwekeza kwenye mitambo hiyo anauhakika wa kuuza tani 20 za sukari kila siku lakini kwa upande wa mtambo wa muhogo tunategemea kuufunga wilaya Handeni kwa kushirikiana na bodi ya mazao mchangayiko,"alisema Prof Kahimba.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko (Temdo) Dkt.Sigisbert Mmasi alisema kuwa uwepo wa teknolojia utaweza kuwarahisishia kaI wakulima wakati wa usindikaji kwani watalazimika kutumia siku moja pekee tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wanantumia siku zaidi ya 10 huku wakitumia nishati ya jua katika ukaushaji.
"Kwa kutumia teknolojia hii mkulima ataweza kuvuna mhogo wake na akaukausha siku hiyo hiyo na akaweza kufungasha unga katika vifungashio tayari kwa matumizi ya nyumbani Mimi nadhani kuwa huyu ni mkombozi mkubwa sana na Sasa tutaweza kutoa thamani halisi ya zao Hilo la mhogo"alisema
Katika hatua nyingine aliwataka wajasirimali ambao ni wamiliki wa viwanda kuhakikisha kuwa wanatumia uwepo wa taasisi hiyo hasa katika uvumbuzi wa mashine na teknolojia mpya ambazo zote zinalenga kuinua uchumi wa taifa
Alisema kuwa huwa wanawawezesha wadau wa viwanda kwa kuwapa elimu na namna sahihi ya kutumia mashine kwa ajili ya matumizi mbalimbali ndani ya viwanda.
"Lengo letu ni kuona kuwa sekta hasa ya viwanda inakuwa na mapinduzi makubwa kwa kuwa tuna uwezo mkubwa sana wa kutengeneza vitu ambavyo hapo awali vilikuwa vinazalishwa nje ya nchi Sasa tunazalisha na kubuni kwa umairi mkubwa,niwatake watanzania na wamiliki wa viwanda Sasa kutumia taasisi hii ili tubuni wote kwa pamoja.
0 Comments