********************
Na Junior Mwemezi Mpanda KATAVI.
Wadau mbali mbali wa kilimo cha Pamba nchini wamekutana mkoani katavi katika kikao kazi cha mradi wa pamba wa Cotton Victoria ambapo kwa pamoja watashirikiana kujadili kazi zilizofanywa na mradi huo kwa kipindi cha mwaka 2021 mpaka 2022 na kuweka mpango kazi wa kipindi cha mwaka 2023.
Akifungua kikao kazi hicho kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa TARI ,meneja wa mipango na tathimini. Dr Deogratias Rwezaula amesema mradi huo unaotekelezwa kwa ushirikiano na nchi ya Brazil umesaidia wakulima wengi wa kanda ya ziwa kulima kilimo cha pamba chenye tija.
Aidha katika kikao hicho mratibu wa zao la pamba nchini anayesimamia mradi huo Dr Paul Saidia ,amesema kuwa mradi huu umesaidia kuinua kipato cha wakulima kwa kuongeza uzalishaji kwani wakulima wamefaidika kupata elimu sahihi juu ya kilimo cha pamba
Amesema kuwa kwa sasa wakulima wamewwza kubadilisha upandaji kutoka sentimenta 90 kwa 40 mpaka 60 kwa 30 ambapo kwa kufanya hivyo inaongeza idadi ya mimea mara mbili na hivyo kuongeza mavuno maradufu.
0 Comments