NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi ametembelea Kata ya Kibosho Magharibi ambapo alikagua mradi wa ujenzi wa Barabara ya Kibosho Umbwe eneo la kwa Edita inayoendelea kujengwa kwa Kiwango Cha lami.
Mradi huo wa Barabara wenye urefu wa mita 425 unatekelezwa na mkandarasi
Kifuko Keko Furniture ambapo Mpaka sasa umefika asilimia 95.
Mhandisi na msimamizi wa barabara hiyo Mhandisi Benedict Charles alisema kuwa mradi huo ulipaswa uwe umekamilika mapema ila changamoto ya mvua imefanya kusimama kwa muda ambapo sasa wako mbioni kukamilisha.
Mhandisi huyo alimweleza mbunge kuwa kwa sasa wako katika hatua ya kuweka mitaro na baada ya wiki tatu kuanzia hivi sasa watakuwa wamemalizia kazi ya kuweka lami.
Mbunge Ndakidemi amefurahishwa na jinsi kazi hiyo inavyokwenda na amemsihi mkandarasi amalize mapema ili wananchi waweze kutumia barabara kama ilivyopangwa kwani sehemu iliyobaki imekuwa ni kero kwa wananchi wa Kibosho Magharibi.
Mwisho
0 Comments