Wananchi wa kijiji cha Igombola kata ya Lupembe Wilaya ya Njombe wamelalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara ya kwenda Zahanati pamoja na maeneo ya vijiji vingine vya kata ya mfiriga kwani imekuwa ikiwakwamisha kiuchumi na kuhatarisha maisha yao.
Katika mkutano wa hadhara wa mkuu wa Wilaya ya Njombe baadhi ya wakazi hao akiwemo Peter Kyamani na Lucy Mligo Wamesema ubovu wa barabara hasa wakati wa masika umekuwa ukikatisha mawasiliano pamoja na mazao kuozea shambani.
Awali diwani wa kata ya Lupembe Michael Mbanga amesema changamoto ya miundombinu ya barabara ni kubwa hususani katika kipindi cha masika kwani shughuli za kiuchumi zimekuwa zikisimama.
Mkuu wa wilaya ya Njombe katika ziara yake ametembelea na kufanya mikutano katika kijiji cha Igombola kata ya Lupembe pamoja na vijiji vya Madeke na Mfiriga kata ya Mfiriga.
0 Comments