Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ameziagiza kamati zote za ujenzi kuharakisha ujenzi wa madarasa kupitia fedha alizotoa Rais Samia Suluhu Hassan siku chache zilizopita ili ifikapo januari mwakani wanafunzi wote watakaofaulu wasikose nafasi.
Kasongwa ametoa agizo hilo leo baada ya kutembelea na kukagua maandalizi ya ujenzi huo katika shule ya sekondari Itipingi kata ya Igongolo ambako tayari zoezi limeshaanza kwa kukusanya tifali na mchanga huku wakiwa kwenye mchakato wa kutangaza tenda ya kumpata fundi.
Awali Mkurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Njombe Sharifa Nabalang'anya amesema halmashauri hiyo imepata kaisi Cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hayo.
Katibu tawala Wilaya ya Njombe Emmanuel George yeye amesisitiza ubora wa kazi pamoja na kuzingatiwa kwa muda wa ukamilishwaji wa ujenzi.
Baadhi ya madiwani wa kata ya Igongolo Isaya Myamba,Peter Nyang'uya diwani kata ya Kichiwa pamoja na wakuu wa shule hizo wanasema wamejipanga vyema kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kabla hata ya muda wa maelekezo ya serikali
0 Comments