Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanali Patrick Sawala ambapo ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania TARI kituo cha Naliendele kwa kazi nzuri za Utafiti ambazo inafanya na hata kuweza kuwavutia watu toka ndani na nje ya nchi kutembelea taasisi hiyo.
Kauli hiyo ameitoa jana ofisini kwake baada ya kutembelewa na watafiti kutoka TARI Naliendele na watafiti kutoka nchini Benin alisema kuwa TARI imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na Wadau mbalimbali wa zao hilo la Korosho katika Wilaya yake wakimwemo Maafisa Ugani pamoja na Wakulima wa zao hilo.
“Nafurahishwa na jitihada kubwa zinazofanywa na tari ni jitihada ambazo zinaonyesha kuzaa matunda sio kwa kwetu hata kwa wageni nchi ya nchi wameona ndio maana wanalazimika kufika katika kituo hicho kujifunza mambo mbalimbali ya kiutafiti”
“Niwatie moyo kazi mnayofanya ni kubwa na inaonyesha matunda kwa wilaya hii tunaona jinsi korosho zinavyofanya vizuir na tunaoufutiliaji wetu unaridhisha” alisema kanal Sawala
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri (W) Tandahimba Bw. Mussa Lawrence Gama halmashauir ambayo inaongoza kwa ulimaji wa zao korosho nchini alisema kuwa anafurahishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo katika wilaya hiyo.
“Hapa kwetu uchumi ni korosho yaani korosho ndio kila kitu tunajivunia kuwa wazalishaji wakubwa lakini tunaouna uthubutu wa wataalamu wetu wamekuwa mstari wa mbele kutusimamia na kutuongoza ndio maana leo mnatuona tunafanyavizuri kwa kufuata ushauri wao na miiongozo ya kitalaamu waliyoiweka” alisema Gama
Katika ziara hiyo pia walitembelea kituo cha uendelezaji zao la Korosho (CDC) Nanyanga kinachosimamiwa na Taasisi hiyo wakiwa na lengo la kujifunza Kilimo bora cha zao la Korosho nchini Tanzania pamoja na Bw Juma Mkumwile lililoko kijiji cha Mnaida Wilaya Tandahimba na kuweza kubadilishana uzoefu lakini pia kujifunza namna bora ya kuhudumia shamba.
MWISHO
0 Comments