********************
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima ameongoza kikao maalumu kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa hatari wa Ebola ambao upo nchi jirani ya Uganda ambacho kimewakutanisha makundi mbalimbali ikiwemo viongozi wa kamati ya amani ya mkoa huo.
Aidha mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima amesema lengo la kukutana kujadiliana kuhusu ugonjwa wa Ebola mkoani Mwanza ni kuweka utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo hatari ambao unaendelea kusambaa kwa kasi nchini Uganda.
Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Lutachuzibwa amesema ni muhimu kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Ebola kwakua umenea kwa haraka nchi jirani ya Uganda huku akisema dalili mojawapo ya ugonjwa ni pamoja na homa kali.
Pia mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Lutachuzibwa amewataka wananchi wa mkoa huo kuepuka safari zisizokuwa za lazima kwenda nchini Uganda ili kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola ambao tayari upo nchini humo.
Dkt. Thomas Lutachunzibwa amesema, ugonjwa wa Virusi vya Ebola huenea kwa mtu mmoja na mwingine kwa njia kama kugusana, matapishi,jasho,mate,machozi,mkojo au kinyesi kutoka kwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo.
Dkt.Lutachunzibwa amewataka wakazi wa mkoa huo kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola kwa kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji yanayotiririka ili kujikinga na ugonjwa huo.



.jpeg)





0 Comments