***********
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza Katibu wa Shirikisho la Walimu Makada wa CCM Devid Sulubhe amesema, katika kuadhimisha mwaka (1) wa Shirikisho hilo watafanya zoezi la upandaji wa miti ipatayo 10,000 ambayo itapandwa wilaya zote za mkoa wa Mwanza kupitia kwa wanashirikisho walioko wilaya hizo na pia shule ya sekondari Lugeye iliyopo wilayani Magu.
Devid Sulubhe amesema, wameamua kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu (6) kufanya shughuli za kijamii katika kuadhimisha sherehe ya kila mwaka ya Shirikisho pia kumkaribisha Mkuu wa mkoa huo Adam Malima.
Sulubhe amesema, katika kuadhimisha mwaka (1) watagawa taulo za kike zipatazo 21,504 zenye thamani ya Tsh.milioni mbili na nusu ikiwa kama kutambua wajibu wa kuilea jamii hususani watoto.
Katibu wa Shirikisho la Walimu mkoa wa Mwanza,Devid Sulubhe amesema, Oktoba 7 watagawa taulo za kike kwa watoto 300 wa kidato cha tano na sita shule ya sekondari Lugeye iliyopo wilayani Magu mkoani humo pia zitagawiwa taulo kwa watoto 150 wenye mahitaji maalumu katika shule sekondari Buhongwa
Mwenyekiti wa Shirikisho la Walimu Makada wa CCM wilaya ya Misungwi Alphonce Kaligilwa amesema, katika kuadhimisha mwaka (1 ) wa Shirikisho hilo Octoba 8 wanatarajia kufanya zoezi la uchangiaji wa damu,kutoa vyakula na vifaa mbalimbali kituo cha afya Buzuruga Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.








0 Comments