Header Ads Widget

MASHINDANO YA TUZO ZA UBORA ZA KITAIFA YAZINDULIWA





Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


WIZARA ya Uwekezaji Viwanda na Biashara, Shirika la Viwango Tanzania TBS  pamoja na sekta binafsi wamezindua Mashindano ya  tuzo za ubora za kitaifa kwa mwaka 2022/2023 .


Tuzo za ubora zilianzishwa ikiwa ni makubaliano baina ya wanachama wa jumuiya ya maendeleo  kwa nchi za kusini mwa Afrika (SADC)ili kutambua na kukuza sekta ya biashara kupitia ubora wa bidhaa .


Akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma Mkurugenzi mkuu Shirika la viwango Tanzania TBS Dkt Yusuph Ngenya alisema kuwa washiriki wa tuzo za ubora za SADC wanapaswa watokane na washindi wa tuzo za ubora za kitaifa.



“ Tuzo hizi ni sehemu mipango ya serikali katika kuboresha huduma na bidhaa zinzotengenezwa nchini kupitia matumizi ya viwango  na kanuni za ubora kwa taasisi  za  umma na sekta binafsi ,”alisema


Na kuongeza “ Lengo ni kuhakikisha kuwa Mifumo ,bidhaa na huduma zinakidhi ubora kitaifa ,kikanda na kimataifa na hivyo kufanya vizuri kwenye masoko ya ngazi zote,” alisema Dkt  Ngenya.


Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wizara ya uwekezaji ,Viwanda na biashara Aristides Mbwasi alisema mashindano ya tuzo hizo yamegawanywa katika vipengele vitano ambavyo  ambavyo Tuzo kwa kampuni ya mwaka , Tuzo kwa bidhaa ya ubora ya mwaka ,tuzo kwa huduma bora ya mwaka ,tuzo kwa Muuzaji bora wa bidha nje ya nchi na tuzo ya mwisho ni Mtu mmoja aliyefanya vizuri kwenye masuala ya ubora.



“kwa kipengele cha kwanza hadi cha nne zimeandaliwa tuzo kwenye makundi mawili kwa kila kipengele yani tuzo kwa kampuni kubwa na pia tuzo kwa wajasiriamali  wadogo wadogo wakati( SME) na kipengele cha tano kinahusisha tuzo kwa mmoja pekee,”alisema Mbwasi


Naye  Mwakilishi kutoka ZBS Hafsa All Salim Mkurugenzi wa Idara ya maendeleo ya viwango akimwakilisha mkurugenzi wa shirika la viwango ZBS alisema kwa upande wa Zanzibar wameshiriki na wanatarajia kutoa uelewa kwa wafanyabishara  na wajasiriamali washiriki kwa wingi  .



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI