Header Ads Widget

MADIWANI NJOMBE DC WACHARUKA KUCHELEWESHWA KWA FEDHA ZA ASILIMIA 5 ZA VIJIJI

 



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Njombe wamelalamikia kucheleweshwa kwa fedha za asilimia 5 za makusanyo ya ndani zinazopaswa kurejeshwa kwenye vijiji ili ziweze kusaidia katika uendeshaji wa majukumu yaliyopo kwa maofisa watendaji.


Hatua hiyo imetajwa kukwamisha jitihada za ukusanyaji mapato zaidi kwa kuwa yanayokusanywa mgao wake haurejeshwi kwa wakati hivyo kuwakosesha molari maofisa watendaji wanaofanyakazi hiyo wakati wote.


Katika mkutano wa baraza la madiwani wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2022/2023 baadhi ya madiwani hao akiwemo Vasco Mgunda,Neema Mbanga  na Paulo Kinyamagoha wamesema kumekuwa na mkanganyiko mkubwa wa asilimia za fedha hizo katika maeneo tofauti na wakati mwingine kucheleweshwa jambo ambalo linakatisha tamaa katika kuongeza juhudi.



Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Ahamad Maguo amesema halmashauri hiyo imekuwa ikitumia kila njia kuhakikisha fedha hizo zinapelekwa kwenye vijiji licha ya kuwapo kwa baadhi ya changamoto.


Akitolea ufafanuzi zaidi juu ya malalamiko ya madiwani hao,mweka hazina wa halmashauri hiyo bwana Madiya Magessa amesema wao wamekuwa wakipeleka fedha hizo kama maelekezo yaliyovyo bila kubagua  maeneo yenye mageti ya kukusanyia ushuru na ambayo hayana huku akikiri kuwapo kwa baadhi ya miezi ambayo fedha hizo hazijapelekwa kwenye vijiji baada ya kufungwa kwa mwaka wa fedha hapo juni na fedha kurudi kuwa bakaa.



Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo bwana Melkizedeck Kabelege amemtaka mkurugenzi kuhakikisha anapaleka fedha hizo kwenye vijiji kwa mujibu wa sheria badala ya kuendelea kukwamisha shughuli za vijiji na kata kwa kuchelewesha fedha hizo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI