Header Ads Widget

YEMCO VICOBA KUUNGANA NA VODACOM KUIMARISHA UTUNZAJI WA FEDHA ZA VIKUNDI

 


Taasisi ya kuweka na kukopa vicoba endelevu -Yemco- imejipanga kuhakikisha inawafikia wananchi wa maeneo ya pembezoni ili kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini sanjali na kuwa tegemezi katika jamii.


Hayo yalisemwa na Rais wa vicoba ambaye pia ni mkurugenzi wa taasisi hiyo Mohamed Basanga katika wiki ya kuondoa umasikini duniani +VICOBA DAY- iliyofanyika jijini Dar es salaam ikiwa ni pamoja na kukutanisha vikundi mbalimbali vya Kuweka na kukopa vilivyo chini ya mwamvuli wa YEMCO na kuendelea kuwahamasisha wananchi kujiunga na vikundi ili kujiwekea akiba na kutimiza malengo yao.


Basanga Alisema kupitia maadhimisho hayo YEMCO imeungana na kampuni ya simu ya mkononi VODACOM ili kurahisisha huduma ya kuweka pesa kwa kutumia umbali mrefu kutokana na baadhi ya maeneo kupata huduma za kibenki kuwa mbali na vikundi vyao.


" Leo tumeungana rasmi na VODACOM kuwasaidia wanakikundi kutumia huduma ya lipa kwa simu kupitia M-MKOBA itawasaidia kuwa na usalama zaidi wa kuhifadhi fedha zao tofauti na kutembea na fedha hizo umbali mrefu ambao kwa wakati mwingine pia sio salama.


Pia  amesema VODACOM M-Mkoba itakuwa suluhu ya kuondoa usiri kwenye vikundi maana mfumo huu utawajulisha wanachama wote pesa inayoingia na  kutoka ."Alisema Basanga.


Basanga amesema lengo moja wapo lakuadhimisha siku hiyo ni kuona namna vicoba vilivyowasaidia wananchi kuondokana na umasikini hivyo kuwaomba wananchi kuendelea kuwa waaminifu na kutimiza malengo yako kupitia vikundi mbalimbali vya kuweka na kukopa.


Naye Beatrice Athony ambaye ni mmoja wa wanakikundi Cha Yemco  Vicoba ilivyomsaidia kutimiza malengo yake" Nilikuwa naogopa kuingia katika vikundi vya mtaani na kuepuka kudhulumiwa ila tangu nimejiunga vicoba  chini ya mwamvuli wa YEMCO Vicoba endelevu nashukuru nimeona mabadiliko katika UTUNZAJI WA fedha  baada ya kupata elimu ya fedha na kutimiza malengo.'"Alisema Beatrice Anthony


Hata hivyo taasisi imeishukuru serikali kupitia mikopo ya halmashauri ya aslimia 10 kwa ajili ya makundi mbalimbali  hivyo kuwaomba wanachama kutimiza vigezo ili kunufaika na fedha hizo


Mwanzoni wanachama walikuwa wanomba mikopo hiyo kwa kufuata hatua mbalimbali za kwenda serikali za mitaa kujaza fomu lakini kwa Sasa imeboreshwa kuingia katika mfumo wa kidijitali na kuhakikisha kikundi kinakuwa na sifa ya kupata mikopo hiyo na mpaka  Sasa Kuna vikundi vimenufaika na mikopo hiyo.'"Alisema Basanga


Taasisi ya Yemco Vicoba mpaka Sasa imeendelea kuhamasisha vikundi zaidi ya 200 vya  kuweka na kukopa kutoka makundi mbalimbali  ndani ya mkoa wa Dar es salaaàm na nje ya mkoa huo.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI