Header Ads Widget

ICGLR YAENDESHA MAFUNZO KWA WADAU WA UCHAGUZI, AMANI USALAMA NA DEMOKRASIA VYASISITIZWA

 


Na fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam


Jumuiya ya nchi za ukanda wa maziwa makuu (ICGLR) kwa kushirikiana na wadau wengine wa uchaguzi wakiwemo Umoja wa mataifa  wameandaa mafunzo ya kuijengea uwezo tume ya Uchaguzi na wadau wa uchaguzi kutoka nchi 12 ambazo ni wanachama wake.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua mafunzo hayo Waziri wa nchi Ofisi Waziri Mkuu,Sera Bunge na Uratibu George Simbachawene amesema pamoja na mambo mengine lengo la mafunzo hayo ni kuwataka wanachama wake waendeleze kuendesha uchaguzi wa  huru, haki na kuaminika.


Amesema kuwa, Ili kuendelea kukuza demokrasia, amani na usalama nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu zinapaswa kuona ipo haja ya kuwa na uchaguzi huru na wa haki unaozingatia usawa kwa wote, ambapo ndio  ambapo ni sehemu ya itifaki ya umoja wa mataifa(UN) inayohusiana na masuala ya Demokrasia na Utawala Bora.


Ameongeza kuwa, miongoni mwa mambo yatayojadiliwa katika warsha hiyo ni pamoja na nafasi za Asasi za kiraia katika kuboresha Ushiriki wa makundi maalum na uadilifi katika uchaguzi kupitia utazamaji wa uchaguzi, elimu ya mpiga kura na elimu ya uraia na changamoto na fursa zilizopo katika kuboresha Ushiriki wa watu wenye ulemavu.


 "Masuala mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo nafasi ya vyombo vya habari katika kuboresha Ushiriki wa makundi maalum na uadilifi katika mchakato wa uchaguzi na kuhakikisha kunakuwa na amani na utulivu, kuboresha uadilifu na uchaguzi unaoshirikisha makundi yote katika jamii kama vile wanawake, wazee, vijana na watu wenye ulemavu"amesema Waziri Simbachawe.


Hata hivyo, amesema kuwa matumizi ya Tehama katika uchaguzi pia yatajadiliwa, pamoja na fursa zilizopo katika kuboresha ushiriki wa vijana katika uchaguzi ama kama wagombea au wapiga kura, ambapo pia wajumbe wa mkutano kujadili  changamoto na fursa zilizopo katika kuborsha suhiriki wa watu wenye ulemavu na wanaoishi kwenye mazingira magumu katika chaguzi mbalimbali.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) Dkt Charles Mahera amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuwajengea uwezo wajumbe na watendaji wa Tume za Uchaguzi za Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.


Aidha, amezitaja nchi kumi na mbili  Wanachama wa Jumuiya ya ICGLR ni pamoja na Tanzania, Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Uganda, Rwanda, Sudani Kusini , Sudani na Zambia, zikiwa na lengo wa kuhakikisha chaguzi zinakuwa huru za haki na zenye kuaminika ili kusaidia kukuza demokrasia itakayochochea amani na usalama.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI