Header Ads Widget

𝗪𝗔𝗞𝗨𝗟𝗜𝗠𝗔 𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗭𝗔𝗢 𝗬𝗔 𝗕𝗨𝗦𝗧𝗔𝗡𝗜 𝗞𝗨𝗝𝗘𝗡𝗚𝗘𝗪𝗔 𝗨𝗪𝗘𝗭𝗢.




Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amesema Serikali inafanya juhudi za kuwawezesha wakulima wa mazao ya bustani kusindika mazao yao ili kuyaongezea thamani kabla ya kuyaingiza sokoni. 


Mhe. Bashe ameyasema hayo jana Jijini Dodoma alipozindua Mkakati wa Kitaifa wa kuendeleza Mazao ya Bustani na Mwongozo wa Usimamizi wa Tasnia ya Parachichi.



Waziri Bashe alisema miongoni mwa changamoto zinazowakabili Wakulima hao ni pamoja na ukosefu wa maarifa na miundombinu ya kuhifadhi na kusindika mazao yao.


Wazir Bashe ameongeza kuwa Wakulima wa Mazao ya Bustani watakapotatua changamoto hizo watakuwa na uhakika wa soko na wataweza kuuza kwa faida.



Aidha Mhe.Bashe ameeleza kuwa Serikali itashirikiana kwa karibu na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Kilimo, Mifugo na Maji katika kutekeleza Mkakati huo.


"Serikali imejipanga kuhakikisha Kilimo hicho kinazidi kusonga mbele, na katika bajeti ya mwakani fedha lazima zitengwe," Alisema Mhe. Bashe.

 


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw.Andrew Massawe amesema maamuzi ya kuuandaa Mkakati huo yametokana na maombi ya Wadau mbalimbali na vikao vilivyofanyika Wizarani.


Ameongeza kuwa Mkakati huo unalenga kutoa msukumo katika kuongeza tija, malighafi za viwanda na masoko ya ndani na nje ya mazao ya bustani.


Alisema uandaaji wake umeshirikisha wataalamu wa Wizara na Sekta Binafsi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS